const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Nape Aibuka Tena leo, Aongelea taarifa zinazomuhusisha yeye na Kinana - HABARI MPYA

..

Nape Aibuka Tena leo, Aongelea taarifa zinazomuhusisha yeye na Kinana


Moja kati ya taarifa zilizosambaa leo katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Abdularahman Kinana kuwa ataongea na vyombo vya habari saa nne asubuhi ofisi ndogo ya chama cha CCM Lumumba Dar es Salaam.
Taarifa hizo hazikuwa za kweli lakini uvumi ukaendelea kuenezwa kuwa Kinana amekatazwa kuongea na waandishi, taarifa ambazo sio za kweli pia huku ikionekana account fake ya Mbunge wa Mtama ambaye ameondolewa katika uwaziri Nape Nnauye ndio kaandika katika twitter account yake.

Hii akifafanua kuhusu ujumbe uliyoenezwa kuwa kamuandikia Kinana
Nape Nnauye ametumia ukurasa wake rasmi wa twitter kueleza kusikitishwa kwake na watu wanaozusha taarifa hizo zenye lengo la kumchafua kuhusu katibu Mkuu wa CCM Kinana, Nape ameandika kuwa hajaandika taarifa hizo zinazomuhusu Kinana.

Kutoka katika twitter ya Nape kuwa ujumbe huu sio wa kwake

TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

Related Posts

Post a Comment