BAADA ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuelezea mafanikio aliyoyapata, changamoto alizokutana nazo na mipango inayofuata ya mwaka wake wa pili aliouanza, wanawake wanaofanya biashara ya ‘uchuuzi wa mwili’ (machangudoa), wameibuka na mbinu mpya ya kumdhibiti kiongozi huyo ili asiwabughudhi.
Uchunguzi uliofanywa na Risasi Jumamosi umebaini kwamba, baada ya kuchoshwa na kukimbizwa na kukamatwa na polisi chini ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro wanapojiuza barabarani kwa amri ya Makonda, sasa wameanzisha mtandao wa kujiuza ambao unaelezwa ni hatari zaidi.
“Unaambiwa sasa hivi mambo ni kidijitali na ni vigumu kuwakamata kwani huwezi kumtambua mwanamke anayejiuza kirahisi kwa sababu mchongo mzima unachongwa mtandaoni kupitia Mitandao ya Kijamii ya Instagram na WhatsApp na siyo kusimama barabarani kama zamani.
“Wenyewe wanasema wamempiga tobo Makonda kwa kubuni njia mpya ya kuwaingizia kipato, tena bila kujidhalilisha kama zamani,” alitonya mtoa taarifa wetu hivyo kutoa ‘asainmenti’ kwa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers.
OFM KAZINI Ikiwa kazini, OFM ilitonywa kuwa kwa sasa kuna mbinu mpya ambayo machangu wanatumia kwa sasa hasa wa maeneo ya Sinza ambao wametoweka katika vijiwe vyao kisha kujituliza magetoni kwao kusubiria oda kutoka kwa wanaume hivyo kuwataka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na polisi kuingilia kati kukomesha ishu hiyo.
“Hivi mnajua kuwa machangu siku hizi hawaonekani kwenye maeneo yao ya usiku? Unajua kuna kipindi walizidi mno lakini kufuatia udhibiti wa polisi chini ya Makonda wa kuwapitia na kufunga maeneo, sasa wameunda magrupu tofautitofauti mitandaoni na kuwavuta wateja wao kirahisi. WANAFANYAJE? ”
Ishu nzima ipo hivi, wanajitangaza kwa kuanika picha zao za utupu na nusu utupu pamoja na vipande vya video kwenye Instagram kisha wanakuwekea namba zao za simu na kukutangazia, ukitaka kujiunga kuwaona live unatuma kiasi cha kati ya shilingi 5,000 hadi 10,000 na ukiingia humo unawakuta kibao hivyo TCRA na polisi kazi wanayo.
“Wapo wanaotoa huduma ya kukuunganisha tena kwa utakayemtaka kwa gharama ya shilingi 10,000 kisha ushindwe mwenyewe tu kwani wapo tu magetoni wanasubiri uingie kwenye kumi na nane zao,” alisema Abdi, mkazi wa Afrika Sana, Dar.
OFM YACHIMBA Baada ya kujua mbinu hiyo, OFM ilijipanga na kumtuma mmojawao ambapo aliingia katika Mtandao wa Instagram na kukutana na makundi mengi ambayo yamewekwa majina ya kukuonesha kuwa huduma hiyo ipo kisha akawatumia kiasi hicho cha fedha na punde akaunganishwa na kushuhudia video na picha za utupu.
MMOJA AINGIA MTEGONI Baada ya kuunganishwa kama yalivyo masharti yao, aliomba apatiwe mmojawao ambapo aliambiwa atoe tena kiasi kingine cha shilingi 10,000 na baada ya kufanya malipo hayo aliunganishwa na mrembo aliyetambulika kwa jina moja la Irene tayari kwa kwenda kujinoma naye.
OFM aliahidiana na Irene kukutana sehemu kwa ajili ya huduma hiyo na kukubali kufika lakini baada ya kuketi katika maongezi, OFM akiwa katika harakati za kuchomoa simu apige picha kadhaa, Irene alishtuka na kuwa mkali kama pilipili ambapo alitaka kumkusanyia watu hivyo OFM kupata wakati mgumu kabla ya mrembo huyo kutimua kwa kumnyeshea mvua ya matusi.
OFM ARUDI TENA KUNDINI Licha ya Irene kushtuka kama anataka kupigwa picha, OFM ilirudi tena katika kundi hilo kwa lengo la kumpata mwingine kwa kuwa alikuwa bado mmoja wa memba hivyo ikawa rahisi kuchukua na namba ya mwingine lakini kila alipokuwa akipigiwa alipokea na kudanganya maeneo alipo.
WASIKIE TCRA Baada ya kujiridhisha kuwepo kwa mbinu hiyo mbadala OFM iliwasiliana na Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy ambaye alisema kuwa, ishu hapo ni kuwe na mtu wa kwenda kulala kwenye Kitengo cha Uhalifu wa Kimtandao cha Polisi (Cyber Crime Unity) ambao hao ndiyo wenye idhini ya kumkamata mtu.
KITENGO CHA CYBER Kuhusu ishu hiyo, kamanda wa kitengo hicho, Mwangasa Joshua aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kupokea malalamiko juu ya biashara hiyo, jopo lake la uchunguzi litakaa na kuyabaini ‘magrupu’ hayo ili kuyachukulia hatua kwani Sheria ya Makosa ya Mtandao ipo na inafanya kazi.
TUJIKUMBUSHE Juni mwaka jana, Makonda alitangaza vita na makakapoa (mashoga) na madadapoa (machangu) walioko jijini Dar kuwa ataendesha msako mkali wa kuwaondoa, jambo lililofanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Credit - Global Publishers
Post a Comment
Post a Comment