Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu ambaye pia alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne, ameguswa na ishu ya kuvamiwa wa kituo cha Clouds Media pamoja na kitendo cha aliyekuwa waziri wa habari Nape kutishiwa bastola ili asiongee na waandishi wa habari muda mchache baada ya kupigwa chini kwenye baraza la mawaziri na nafasi yake kuchukuliwa na Harrison Mwakyembe.
Wabunge wengi wa CCM walikuwa kimya dhidi ya sakata hilo ambapo Ijumaa hii, Nyalandu ametaka matukio hayo kwenda kujadiliwa bungeni.
Kupitia twitter mbunge huyo alitweet,”IMESIKITISHA sana kuona AFISA akimtishia silaha Waziri Mstaafu Nape.Kitendo hicho ni kinyume na maadili ya TAIFA letu na kimedhalilisha NCHI,”
Aliongeza, “Kupitia BUNGE, nitaiomba SERIKALI ichukue HATUA za kinidhamu na kisheria DHIDI ya AFISA aliyemtishia Mh NAPE kwa SILAHA.Kitendo HAKIKUBALIKI,”
Katika sakata la RC Makonda kuvamia kituo cha Clouds Media alitweet, “Katika kutekeleza wajibu wake KIKATIBA, BUNGE ni sharti lijadili na kutoa AZIMIO kuhusu kilichojiri CLOUDS FM, na UHURU wa VYOMBO vya HABARI,”
Pia kitendo hicho kimeweza kupingwa na mashirika mbalimbali habari nchini.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
Post a Comment
Post a Comment