Hapa sikutaka kumzungumzia kabisa Makonda hata nilipokuwa Dodoma kwenye mkutano baadhi ya marafiki tuliosoma nae ushirika tulijadili na kuona chama kinamlea vibaya sana.
Leo nimeona video ikimuonyesha akivamia ofisi za clouds Tv hili jambo ni gumu sana sana Mhe. Rais aliangalie kwa kina sana la sivyo linaendelea kutuchafua sana, ukitazama mitandao ya kijamii utaona tunavyotukanywa na mtu anayeonekana mbaya ni Rais wangu.
Nemeona mandiko baadhi ya makada wenzangu wabunge na hata mawaziri wakishanga jambo hili, mimi binafsi nimeshindwa kuvumilia namuomba Rais wangu na mwenyekiti wangu wa ccm amuondoe Poul Makonda kwenye nafasi hii ya mkuu wa mkoa kuendelea kumwacha ni kukichafua chama chetu.
Makonda Ondoka Mwanyewe kaka yangu na rafiki yangu ondoka mwenyewe kuendelea kubaki ni kuifanya ofisi ya Rais inapoteza dira yake na mwelekeo.
ni mimi
Meijo Laizer
Mjumbe wa NEC TAIFA
Wilaya ya Siha
Post a Comment
Post a Comment