Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi Nape Nnauye amewataka wanachama wa CCM na watanzania kwa ujumla kutulia kwa wakati huu kwani atakutana na waandishi wa habari na kuelezea yote haya yaliyotokea.
Mbunge Nape Nnauye ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika ujumbe unaosomeka, “Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!.
Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!— Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) March 23, 2017
Nafasi ya Dkt Harrison George Mwakyembe imejazwa na Prof. Palamagamba Aidan Kabudi ambao wote wanatarajia kuapishwa kesho.
Post a Comment
Post a Comment