Ruge: Niliwambia SHILAWADU siku ya Alhamisi mchana kuwa wasiirushe 'Story' bila kuongea na upande wa pili (wa Gwajima)
Ruge: Niliwambia Vijana wa SHILAWADU kuwa 'Story' kama ndo anayoisubiri RC basi ajue haitaenda hewani hata kwny Social Media
Ruge: Ijumaa niliwasisitiza SHILAWADU kuwa kipindi kile kisirushwe kwakuwa 'Story' haiko balanced
Ruge: Ijumaa saa 5 kasoro usiku nilipigiwa simu kuwa RC Makonda alikuwa kaja ofisini akiwa na maaskari wakiwa na silaha
Ruge: Nilimpigia simu RC Makonda kumhoji kwanini aje ofisini na maaskari wenye silaha? Akauliza kwanini nimezuia kipindi kuruka!?
Ruge: RC Makonda alikata simu, lkn nilipaniki nikiwazia hizo silaha walizokuja nazo ofisini. Makonda alikichukua kipindi kwny flash
Ruge: RC Makonda alisema "Bahati yenu" baada ya kujua kuwa waliokataa vijana wa SHILAWADU sio waliozuia kipindi isipokuwa mimi
Ruge: Nilimwambia Mkurugenzi wa Clouds(Kusaga) kuwa RC alitukosea heshima; kulikuwa na haja gani aje na silaha na ni rafiki yetu?
Ruge: Ukweli hakuna aliyepigwa ila kulijengwa hofu kubwa kwa wafanyakazi wa Clouds Media. Si jambo dogo hili!
Ruge: Tusikwepe ukweli kuwa sisi Clouds Media kama chombo cha habari tuna wajibu wa ku-balance story. Sijawahi kulazimishwa story...
Ruge: Kuacha shughuli za kazi, Makonda amekuwa akija hapa Clouds kama rafiki. Ila kitendo cha kuja na walinzi kiliwashtua walinzi
Ruge: Kama watanzania, hatutaki kuiona bunduki mitaani. Hili limetokea kutufungua macho kujua ma-RC na ma-DC wanavyofanya kazi yao...
Ruge: Sisi tuhukumiwe kama taasisi, wafanyakazi wetu wasitiwe hofu. Mimi sikuwekwa ndani, nilienda Polisi kuripoti suala hili
Ruge: Mtu akikosea kabla hatujaangalia cheo chake, tuangalie makosa yake. Si kudai eti wanaomkosoa wanapingana Vita ya #DawaZaKulevya
Ruge: Mtu kuwa na nafasi ya Uongozi flani si sababu ya 'kuwapanda' watu . All we want is RESPECT!
Ruge: Video clips za CCTV zinazozunguka mtandaoni kweli ni za hapa Clouds Media. Sisi tulidhani Makonda angeomba radhi kwa kadhia hii
Ruge: Siujutii ukaribu wangu na Makonda. Hata akirudi akaomba radhi bado nitamfikiria! Tunataka kuendelea kumpa ushirikiano
Ruge: Niseme, urafiki na BUNDUKI siutaki. Wanaodai Makonda alikuja hapa Clouds akiwa rafiki wanapotosha! Ametumia vibaya madaraka
Ruge: Clouds inalaani kilichotokea, na inaomba Vyombo vya Habari vitoe ushirikiano ktk kukemea hili. Hatutaki kugombana na Serikali
Tazama Video:
Post a Comment
Post a Comment