Faida Za Mti Wa Mlonge


Mlonge, mlongo, mronge, mrongo, mkimbo au mzunze (Moringa oleifera) ni mti wa jenasi pekee, Moringa, ya familia Moringaceae.

Asili ya mti huu ni Uhindi lakini sikuhizi upandwa mahali pengi pa kanda za tropiki na nusutropiki.

Hutumika kwa


  • kulisha mifugo, 
  • chakula cha watu,
  • kuboresha mashamba, 
  • kusafisha maji ya kunywa
  • mitishamba. 



Majani yake ni chakula bora (mboga chungu), lakini maganda mabichi, maua, mbegu, mafuta ya mbegu na mizizi hulika pia.

Watafiti wa sayansi na tiba wamegundua kuwa mti huitwa mlonge ambao kwa Kiingereza unaitwa Moringa Oleifera una uwezo wa kutibu maradhi mengi katika mwili wa mwanadamu

Nimesikia mengi kuhusiana na mti wa Mlonge lakini hii ni kali zaidi CAPE TOWN, (IPS).
Wakati tatizo linalipolikabili Bara la Afrika, watu wanaangalia uwezekano wa kupata misaada kutoka kwenye mashirika ya kimataifa kutoka nje ya bara hilo.

Lakini hali ya ukame inayoongezeka kwa kasi, miti yenye kuhimili ukame huku ikiwa na majani yenye viini lishe vingi inaweza kuwasaidia watu maskini, pia maeneo ya usalama wa chakula na utapiamlo, wao wenyewe.

Shamba lenye hekta 15 lilipandwa miti ya Mlonge au wengine huuita mti wa miujiza ambao kwa Kiingereza unaitwa Moringa Oleifera, tayari umeshaanza kuleta mabadiliko katika jimbo moja maskini zaidi la Afrika Kusini la Limpopo.

Majani ya Mlonge yamepachikwa jina la chakula chenye viwango kwasababu wanasayansi waligundua yana kiasi cha madini ya


  • Kalisium yanayoweza kupatiakana katika glasi nne za maziwa, 
  • kiasi cha vitamini c inayopatikana kwenye machungwa saba, 
  • Potasium ya kwenye ndizi mbivu tatu. 
  • Pia unapata kiasi cha madini ya chuma mara nne zaidi.



KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi Mlonge unaweza kuwa unaongoza.

Kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu.

Majani ya Mlonge yanaweza


kutafunwa mabichi,
yaliyochemshwa kama mboga au
yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga.



Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika moja lijulikanalo kama Trees For Life,
These tiny leaves could save millions of lives.

Majani ya Mlonge yana


  • Vitamin A nyingi kuliko karoti, 
  • vitamin C nyingi kuliko machungwa
  • madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, 
  • halikadhalika ubora wa protini yake ni bora kushinda maziwa na mayai.



Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha


madini ya chuma (Iron),
kasiamu (Calcium) na
vitamin nyingi za aina mbalimbali,

majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.

Ili kutengeneza ‘tonic’,


saga majani mabichi ya Mlonge pamoja na maji,
yachuje kisha
changanya na maziwa halisi.



Inaelezwa kuwa juisi ya aina hii ni dawa nzuri kwa waja wazito, kwani


huboresha njia ya uzazi na
kumuwezesha mama kuzaa bila matatizo na
kuondoa matatizo baada ya kujifungua.



Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mti wa Mlonge unatibu karibu magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwemo yale magonjwa sugu, baadhi yake ni kama haya yafuatayo:

Mlonge unaweza kutibu


  • Pumu, 
  • Kikohozi
  • Kifua Kikuu.



Aidha, magonjwa mengine kama


Kisukari,
Shinikizo la damu (la juu na chini),
magonjwa ya ngozi,
magonjwa ya kwenye njia ya mkojo (UTI)
kuongeza kinga ya mwili (CD4)
kuongeza nguvu za kiume



FAIDA ZA MBEGU ZA MLONGE
Mbegu za Mlonge hutibu maradhi pia kama


  • Malaria, 
  • Saratani ya tumbo, 
  • hupunguza sonona stress,
  • huleta hamu ya kunywa maji, jambo amabalo ni adimu kwa watu wengi



Mbegu hizo za mti huo wa ajabu bado zinahamasisha jamii kuamka na kuutambua umuhimu wa mti MLONGE kwa mbegu hizo hutoa


mafuta ya kupikia pamoja na
mafuta ya kujipaka mewilini kwa nyakati tofauti.



Kwa upande wa mafuta ya kupikia chakula wataalam anasema mafuta yake ya kupikia


huua sumu kwenye chakula yaani Bacteria na
huondoa cholesterol.


Mafuta ya kupaka mwilini yaani (Moringa Skin Care Oil).

Mlonge unaendelea kutoa faida kemkem kwa mtanzania na jamii yote duniani kwani umeweza kuwapendelea na wanamichezo kwa kutoa mafuta ambayo yanachua pindi mchezaji anapokuwa ameshikwa na misuli wakati akiwa anacheza,

wataalam wanaainisha kwamba katika utafiti wamefanikiwa kutambua faida nyingine ya matumizi ya mti huo baada ya kufanikiwa kutengeneza mafuta ya kuchua na kuondoa maumivu yatokanayo na kukaza kwa misuli ya mwili yaani (MORINGA MASSEGE OIL)ambayo


  • huondoa maumivu ya mgongo, 
  • kiuno, 
  • miguu, 
  • hutibu baridi, na 
  • hupasha misuli joto



Maganda(magome) ya Mlonge husaidia


kusafisha maji(water treatment).



Mizizi hutumika kutibu watu walio na


malaria sugu au
watu wanaopata homa ya usiku au
wanaotiririka sana jasho wakati wa homa.


Mizizi hutumika kwa kusaga unga wake na kutumia kijiko cha chai mara tatu kwa siku.

Tumia mbegu 3x3 muhimu kila ukitafuna mbegu tatu kumbuka kutumia maji glass 3 au zaidi)

Ndugu tuna tabibu mbalimbali, za asili na zisizo na madhara kama ya vidonge vya makemikali na bado tunapuuza.

TIBA NA MBOLEA KWA MIMEA
Watafiti pia wamegudua kuwa majani ya mti wa mlinge yanaweza kutumika kama mboea shambani kwa mimea ya aina zote kutokana na viinilishe na virutubisho vilivyomo katika mmea huu,lakini pia

mizizi yake inapotambaa huambukiza virutubisho kwa mimia iliyo jirani katika eneo la mita tano za mraba ulikopandwa mti wa mlonge.

Related Posts

Post a Comment