Bamia ni zao ambalo lina faida lukuki katika ulimwengu wa kibiashara. Wapo wakulima mbalimbali ambao wamekuwa wakinufaika na zao hilo.
Lakini ukitazama katika sura nyingine bamia zina faida nyingi sana kiafaya hasa pale mtu ambapo anapozitumia, na faida hizo husaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza na kutibu maradhi mbalimbali.
Na Kwa mujibu wa mtandao wa healthandcure.com uliwahi kuwanukuu baadhi ya wataalam wa afya wakieleza kwamba watu wanaosumbuliwa na maradhi ya:
1. mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.
2.Aidha, faida nyingine zinazotokana na ulaji wa bamia ni pamoja na kuwa chanzo kizuri cha vitamin A,
3. Ulaji wa bamia husaidia kuboresha uwezo wa macho kuona vizuri.
4. Vilevile bamia inasaidia kuweka vizuri kiwango cha sukari mwilini.
5. Mbali na hayo, bamia pia husaidia kulainisha choo.
6. Bamia husaidia sana kwa mtu mwenye matatizo ya kula.
7. bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa ya figo, saratani pamoja na pumu.
Hayo ni baadhi ya maajabu ya magonjwa ambayo yanawezwa kutibiwa na ulaji wa bamia, hivyo ni vyema ukatumia bamia mara kwa mara kwa kuimarisha afya yako.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI
Post a Comment
Post a Comment