Mwanamuziki Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz amejitokeza na kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenye vita yake dhidi ya dawa za kulevya aliyoinzisha jijini hapa.
Akizungumza katika matukio mawili tofauti, Diamond alisikika akisema kuwa, Paul Makonda ni mtu ambaye ni jasiri aliyethubutu kufanya kitu ambacho watu wengi na kwa miaka mingi tumekuwa tukiogopa kukifanya.
Suala la kutaja hadharani majina ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya sio jambo dogo, wangapi walikuwepo na wakaondoka bila kufanya jambo lolote. Hivyo kiongozi wa mkoa kudhubutu kusimama, kuwataka na kuanza kuwashughulikia ni hatua ya kupongezwa sana, alisema Diamond.
Mimi simtetei Makonda kwa vile ni mlezi wa WCB, ninaongea kwa sababu najua madhara ya dawa hizi kwa vijana na kwa sanaa yetu.
Leo katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa uongozi wa Makonda, Diamond Platnumz alimwambia RC Makonda kwamba asijali aendelee kupigana kwa sababu ukiona mtoto anapiga kelele basi ujue viboko vimemkolea.
Post a Comment
Post a Comment