const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); CCM SASA KUWAADHIBU PAUL MAKONDA NA ALEXANDER MNYETI - HABARI MPYA

..

CCM SASA KUWAADHIBU PAUL MAKONDA NA ALEXANDER MNYETI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole amesema taratibu zitafuatwa kuwawajibisha viongozi wake na wa serikali wanaokabiliwa na tuhuma na madai mbalimbali.
Polepole alisema hayo jana katika makala ya kinagaubaga, kipindi kinachorushwa na Idhaa ya Kiswahili ya Deuteschen Welle (DW) baada ya kuulizwa swali kuhusu chama hicho kulea utovu wa nidhamu wa makada wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti wanaotuhumiwa kulidhalilisha bunge, na chombo hicho kwa kauli moja kutaka wajieleze.

Makonda na Mnyeti wanadaiwa kulidhalilisha bunge baada ya kutoa kauli za kuwakejeli wabunge kuwa wanalala bungeni na wengine ni wachekeshaji hali iliyosababisha bunge kuunda kamati ya kuwachunguza na kuwataka kwenda mbele ya chombo hicho kujieleza.

Akajibu swali hilo polepole alisema, ninyi hamkujua kama tunawachukulia hatua kwa namna tumewachukulia watu juzi, serikali ina utaratibu wake, Buge lina utaratibu wake na chama kina utaratibu wake. Tunao utaratibu tunaofuata, wananchi wawe na subira.

“Wananchi wawe na subira, ninafahamu wananchi wana subira sana, wasubiri Mamlaka za viongozi, hawa wote waliokosea, mchakato wa haki ufanyike na hatimaye tutaona matunda yake.”

Hapa chini ni sauti ya Polepole akifanya mahojiano na DW.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://www.androidcreator.com/apk/app221302.apk
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


Related Posts

Post a Comment