Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amefunguka kwa kudai kuwa yeye ni mmoja kati ya mashabiki wakubwa wa msanii Harmorapa ambaye anafanya vizuri na wimbo wake ‘Kikobo ya Mabishoo’.
Rapper huyo amesema kuwa yeye kwenye playlist yake ya kila siku lazima asikilize wimbo wa rapper huyo.
“Nampenda sana Harmorapa na mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao nasikiliza sana kazi zake, hata wimbo wake mpya uko kwenye simu yangu na kila siku nausikiliza,” alisema Dogo Janja.
“Harmorapa ni msanii ambaye ukimsikiliza unafurahi tu, dogo ni mpambanaji kwa sababu unaona toka amenza mpaka sasa anaende poa kabisa. Kwahiyo mtu akimzungumzia vibaya sijui namwonaje kwa sababu dogo amejaribu na ameweza kufanya kitu fulani,”
Kwa upande wa muziki wake Dogo Janja amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wake mpya hivi karibuni.
Post a Comment
Post a Comment