Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam na Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia

Mwanasheria mkuu wa Malaysia, anasema wanawake wawili wanaodaiwa kumuua ndugu wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un watashtakiwa kwa makosa ya mauaji.
Wawili hao, raia wa Indonesia na Vietnam wanakabiliwa na hukumu ya kifo, kwa mauji ya Kim Jong Nam katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpar.
Malaysia inasema, Bwana Kim aliyekuwa mkosoaji wa nduguye, aliuwawa kwa kutumia sumu aina ya , VX, ambayo imepigwa marufuku na Umoja wa mataifa.
Washukiwa hao wawili wanadaiwa kumpaka usoni kemikali hiyo ya sumu katika uanjwa wa ndege wa Malaysia mapema mwezi huu.
Wamesema kuwa walidhani walikuwa wakifanya mzaha katika filamu.
Post a Comment
Post a Comment