const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); VIONGOZI WA USHIRIKA WILAYANI LIWALE MATATANI - HABARI MPYA

..

VIONGOZI WA USHIRIKA WILAYANI LIWALE MATATANI




Mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe. Sarah Chiwamba

Viongozi wa chama cha ushirika Mahonga wilaya Liwale mkoani Lindi Imani Mtesa katibu mkuu Isa Mpunja katibu msaidizi , Saidi Linda mwenyekiti wa chama na Modester Makota Makamu mwenyekiti wa chama hicho wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya agizo la mkuu wa wilaya Sarah Chiwamba kutaka washikiliwe kwa kosa la kutowalipa wakulima wa korosho zaidi ya 100 wakati minada yote imelipwa katika chama hicho.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakulima wa korosho wa chama hicho kuandamana hadi ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo , kuulalamikia oungozi wa chama hicho kutowalipa fedha zao za korosho msimu 2017/18

Related Posts

Post a Comment