const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Kesi ya Maxence Melo yaahirishwa baada ya Wakili wa Serikali kuomba muda wa kujipanga - HABARI MPYA

..

Kesi ya Maxence Melo yaahirishwa baada ya Wakili wa Serikali kuomba muda wa kujipanga

Kesi namba 457 inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Ndg Maxence Mubyazi Melo imeahirishwa tena baada ya Wakili wa Serikali Bwana Salumu kuomba muda wa kujipanga kwakuwa ametoka likizo.
Aidha kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 13 March 2017 itakapoanza kusikilizwa rasmi kwakuwa upelelezi umekamilika.

Ndugu Maxence Melo amewakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya(Kiongozi wa jopo hilo), Wakili Peter Kibatala na Wakili Omar Msemo.

Katika kesi namba 457, ilielezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwambapa kwamba, katika siku na tarehe tofauti kati ya Mei 10, 2016 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni ndani ya Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Melo akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media Co. Ltd ambayo inaendesha mtandao wa JamiiForums, wakati akijua kwamba Jeshi la Polisi Tanzania linafanya upelelezi wa jinai kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa kwenye mtandao wake, kwa nia ya kuvuruga uchunguzi, alikaidi kwa makusudi amri ya kutoa taarifa ambazo alikuwa nazo, kinyume na kifungu cha 22(2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cyber Crimes Law) namba 14 ya mwaka 2015.

Related Posts

Post a Comment