const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); ZITTO KABWE ASAKWA NA POLISI KWA UCHOCHEZI DHIDI YA RAIS MAGUFULI. ISOME HOTUBA ALIYOITOA - HABARI MPYA

..

ZITTO KABWE ASAKWA NA POLISI KWA UCHOCHEZI DHIDI YA RAIS MAGUFULI. ISOME HOTUBA ALIYOITOA




Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe anasakwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za uchochezi dhidi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Kiongozi huyo anayedaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara wakati akimnadi mgombe Udiwani katika Kata ya Isagehe mjini Kahama, imeelezwa kuwa yupo salama na bado hajakamatwa.

Chama hicho kimetoa taarifa kuhusu sakata zima na kuchapisha hotuba aliyoitoa Zitto Kabwe inayodaiwa kuwa ni ya kichochezi.

Hapa chini ni taarifa kutoka chama hicho kuhusu sakata zima la kutafutwa kwa Zitto Kabwe iliyotolewa jana.

Tunawajulisha kuwa Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe, Mb hajakamatwa na polisi na yupo salama hapa hapa nchini.

Jana tarehe 21/1/2017 Polisi wilayani Kahama wakiwa na magari 7 Kati Yao 4 ya FFU na mabomu ya machozi walivamia Mkutano wa Kampeni wa Chama katika kata ya Isagehe, Halmashauri ya Mji wa Kahama. Kiongozi wa Chama alikuwa jukwaani wakati polisi wanafika na aliendelea na hotuba yake mpaka mwisho na kumnadi Mgombea ndg Ibrahim Masele. Baada ya kushuka jukwaani, Kama kawaida yake KC (Kiongozi wa Chama) alipeana mikono na wananchi na baadaye alipotea katika eneo Hilo.

Polisi waliingia mkutanoni na kuanza kumtafuta KC lakini hawakuweza kumpata na hivyo kumkamata dereva wa Gari alilokuwa anatumia KC ndg Patrick Muhidin pamoja na katibu wa Chama Wa jimbo la Kahama ndg. Vincent Ikerenge. Wote walipelekwa kituo cha polisi Kahama na kuandikishwa maelezo. Gari hiyo Landacruiser V8 imeshikiliwa na polisi mpaka sasa.

Mnamo saa mbili na dakika 2 usiku Polisi walivamia makao makuu ya kampeni ya Chama na kufanya upekuzi mkubwa wakimtafuta KC bila mafanikio. Baadaye waliweka mazuio ya njia zote za kutoka Kahama wakiamini kuwa KC atakuwa anapanga kutoroka na kutoka nje ya Kahama.

Tunapenda kuwajulisha kuwa KC yupo salama na yupo Kahama anasimamia ushindi wa kura. Amewaeleza viongozi wa Chama kuwa Polisi wataweza kumkamata iwapo yeye atataka kukamatwa na sio kwa kuvamiwa bali kwa kuitwa rasmi polisi na kuelezwa makosa aliyoyafanya.

Chama kimefuatilia kujua ni kwanini polisi wanamtafuta KC. Tumejulishwa na polisi kwamba KC Ana mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi katika hotuba zake za kampeni katika kata ya Isagehe Jimbo la Kahama Mjini. Polisi wanasema KC amemchonganisha Rais na wananchi kwa kusema kuwa Rais anakula bure na kulala bure Ndio maana hajali Hali Ngumu ya Maisha ya wananchi wakati huu wa balaa la njaa.

Chama kinalitaka jeshi la polisi kufuata taratibu za kukamata raia kwa mujibu wa sheria na pia protokali za kuwaita polisi viongozi wa Kitaifa Kama ilivyo kwa ndg Zitto. Chama kinajiandaa na wanasheria wake ili kwenda na KC kituo chochote cha polisi nchini Mara watakapopata wito wa kwenda polisi.

Chama chetu kitaendelea kukosoa vitendo vya serikali vinavyoenda kinyume na sheria na desturi ya demokrasia ya Tanzania. Wito wetu ni kwa Serikali kuachia vyama vya siasa na wanasiasa wa upinzani kufanya kazi zao bila bugudha na kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu.

Kiongozi wa Chama anawataka wanachama wote wa ACT Wazalendo kuishi kwa mujibu wa Ahadi 5 za mwana ACT Wazalendo na kusimama kidete kulinda demokrasia ya vyama vingi nchini ambayo ipo hatarini tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani mwaka 2015.

Msafiri A Mtemelwa
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo
Kahama, 22/1/2017

————
Hotuba aliyotoa Zitto Kahama tarehe 7/1/2017 na kuitwa ni uchochezi hii hapa

Nimalizie kwa jambo la mwisho kubwa sana la kitafa lakini si kubwa sana

Leo hii sisi tupo hapa tunaongea na ninyi kwa sababu kuna uchaguzi mdogo Mwaka Jana mwezi Wa Sita Mkubwa mmoja alikuja na amri ya kuzuia mikutano ya hadhara mpaka 2020 hakuna mikutano ya hadharavyama vya siasa vimeundwa na katiba na sheria na inaturuhusu kufanya mikutano

Tusipofanya mikutano ninyi mtajuaje kama chama tawala kinavurunda,? Ndiyo maana ya mfumo Wa vyama vingi lakini bwana Mkubwa yule akazuia mikutano na baadhi ya watu wakamuunga mkono.

Lakini mungu nae ana yake kuna kampeni je atazuia mikutano ya kampeni? Mungu amemuonyesha kuwa kuna Mkubwa zaidi yake licha ya yeye kuwa Mkubwa katika nchi yake

Lakini wananchi kwanini haki hii ya kiraia zikanyagwe,Rais anapata wapi uwezo huu Wa kusema hakuna kufanya siasa wapi anapata halafu viongozi wengine wanamuangalia

Haki ya kufanya mikutano ni haki yetu ya kikatiba haipaswi tusubiri chaguzi ndogo ndiyo tuje kuzungumza na ninyi.

Lazima tuje kuwaambia mambo yanapokuwa hayapo sawa leo vyakula vimepanda bei ukame unakuja kuna baa la njaa tunasema kwa kuwa kuna uchaguzi Mdogo,kama hakuna mambo haya tusingeyasema eti kwa kuwa bwana Mkubwa mmoja kaamua.

Leo hii kuna wabunge wamewekwa ndani miezi na dhamana haitoki kila siku mbunge anapelekwa mahakamani na kurudishwa tu hakuna dhamana

Huyu mtu amechaguliwa na watu wake wananchi zaidi ya laki tatu lakini huyu mtu mmoja kwa kuwa ana jeshi,Magereza usalama Wa Taifa mizinga na risasi mahakama unamchukua kiongozi huyu kutoka Magereza unampeleka mahakamani na kumrudisha mahabusu kisa unamkomoa

Leo inawezekana tukaliona hili ni sawa kwa sababu kafanyiwa mtu Wa chama kingine kafanyiwa Lema ni Wa Chadema eti haituhusu!

Ninawaambia.wakifanikiwa kwa Lema watafika kwa kila mmoja wetu na wote tutawekwa ndani kama hatukemei mambo haya lakini haya yanafanyika hata viongozi wastaafu nao hawastuki wamekaa kimya

Ndugu zangu wana Isagehe juzi Rais alikuwa Bukoba ambapo watu wameharibikiwa Nyumba zao wamepoteza ndugu zao na mbaya zaidi wananchi mbali mbali wakawasidia lakini Rais badala ya kuwafarriji anawaambia kila mmoja atabeba mzigo wake haya si maneno ya kiongozi Wa serikali kuwaambia watu wake

Niwakumbushe tulikuwa na mtu anaitwa Cleopa Msuya katika bajeti ya kwanza ya Rais Mwinyi Msuya akiwa.Waziri Wa.fedha akazungumza bungeni kuwa halo ngumu kila mmoja aubebe mzigo wake huyu aliondolewa ofisini baada ya Siku tatu

Mnamkumbuka Mramba aliposema watanzania watakula majani ilimradi ndege inunuliwe leo yupo wapi?

Leo Rais anaenda Bukoba anawaambia kuwa ni watu Wa majanga tu kwamba tetemeko.lao ukimwi wao kunyauka migomba no wao na kisha anawaambia wataubeba mzigo wao hii si kauli ya kiongozi.

Sisi watanzania tumeumbwa na viongozi wetu wameumbwa kuwa wanyenyekevu,ndiyo maana ninashaangaa Mwinyi yupo wapi?,Mzee Mkapa yupo wapi Kikwete yuko wapi kwanini wako kimya

Viongozi wastaafu wako wapi kumuonya huyu Rais Magufuli ambaye anashindwa kuwa mnyenyekevu mbele ya wananchi waliompa kura huyu anakula Burr,anavaa bure analala bure kwa kodi zetu sasa madaraka yamempanda kichwani.

Related Posts

Post a Comment