WANANCHI Mkoani Njombe wamesema kuwa wanamsuburi kwa hamu
waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa ili wamweleze kero zao na kuwa wamejiandaa
kumpokea itakapo fika zamu yamo Njombe mjini baada ya kuahirishwa kwa ziara
yake.
Wananchi hao wanakua na hamu ya kumsikiliza Waziri Mkuu na
kuwa alipo kuwa ameahirisha ziara yake mkoani Njombe ambapo wakazi wa Mjini
Njombe ilikuwa waziri mkuu azungumza nao Januari 22 mwaka huu.
Wakazi hawa wanasema kuwa wanayo mengi ya kumueleza waziri
mkuu na wanasema kero ya maji, na watumishi wasio jali wateja wao wanatarajia
kumueleza Waziri Mkuu atakapo wafikia.
Wananchi hao wanaomba waziri mkuu atakapo fika Mjiji Njombe
atumbue majipu yanayoisumbua jamii ya wakazi wa mji huo.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri anatoa taarifa kwa
wakazi wa Wilaya yake katika halmashauri mbili za Mji na wilaya.
Hata hivyo Msafiri anaongeza kuwa Waziri mkuu akiingia
wilayani kwake atatembelea kiwanda cha chani na kuzungumza na wakulima wa chai.
Post a Comment
Post a Comment