const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Wakulima wanne washambuliwa kwa Marungu,Sime na wafugaji - HABARI MPYA

..

Wakulima wanne washambuliwa kwa Marungu,Sime na wafugaji

Diwani wa kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya ,akizungumza jambo na baadhi ya wananchi wa kijiji cha kwakonje baada ya kutokea vurugu baina ya wakulima na wafugaji .(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Kibindu
WAKULIMA wanne wamenusurika kifo huko kijiji cha Kibindu kata ya Kibindu,Chalinze,wilayani Bagamoyo baada ya kupigwa na wafugaji kufuatia vurugu kubwa iliyotokea baina yao.
Aidha vijiji vyote vinne vya kata hiyo,vimevamiwa na wafugaji wapya kutoka wilaya ya Mvomero,Kilindi,Kilosa na Handeni hali inayosababisha baadhi ya wakulima kuliwa mazao yao na kuishi kwa hofu hatimae kukimbia makazi yao.
Diwani wa kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya,alisema tukio hilo,limetokea usiku wa kuamkia jan 10,ambapo  wakulima wa familia moja walipigwa maeneo mbalimbali ya mwili kwa visu, marungu na sime .
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Omary Mwemsala,Zaina Rajabu Pelembo,Salama Omary,Walivyo Omary (18)ambao wamelazwa katika hospitali ya Bwagala iliyopo Tuliani mkoani Morogoro.
Mkufya alieleza kuwa Walivyo Omary aliruhusiwa kutoka hospitalini jan 11 baada ya kupatiwa matibabu huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu kutokana na hali zao kubwa mbaya.
“Zaina alipigwa kisu cha kwenye titi na kuvunjwa mkono ambako inadaiwa anajumla ya majeraha sita,na Omary Mwemsala amepigwa na rungu kichwani na kujeruhiwa shingoni baada ya mshikemshike wa kujinasua asichinjwe”alisema Mkufya.
Alieleza kwamba hali ni mbaya kwani wafugaji hao wamekuwa kama wanyama ,hawana huruma na sasa wameamua kuwadhuru wakulima ili mifugo yao ipate malisho.
Hata hivyo Mkufya alisema wafugaji wameingia kwenye maeneo vijiji vyote vya Kwamduma,Kibindu,Kwamsanja na Kwakonje na kugeuza machungio.
“Hali ni tete sana,hiki ni kipindi cha kutayarisha mashamba na kupanda mazao lakini kuna ashilio baya kushindwa kulima kwa kuogopa mazao yataliwa”alisema Mkufya.
Alisema wamechukua hatua ya kufikisha taarifa polisi kata ya Mbwewe ambao wameonyesha ushirikiano wa kufuatilia suala hilo na wanaendelea na juhudi za kuchunguza tukio hilo.
Mbali ya hayo alisema kwasasa wafugaji hao wavamizi,wakikuta kibanda kilichoezekwa na nyasi wanaezua na kulisha ng’ombe wao na mtu mwenye kibanda chake akiuliza anapigwa .
Mkufya alibainisha,pia wanaiba mifugo ya wakulima wanaofuga kisasa kwani  ng’ombe 41 wameibiwa na mbuzi  zaidi ya 30 ,wanaiba kwa kuwaswaga na ng’ombe wao pamoja na kutokomea nao.
Mkufya aliiomba wizara ya mifugo na kilimo kutupia macho migogoro hiyo kwa kuweka sheria kali dhidi ya pande hizo ili kudhibiti matukio ya aina hiyo.
“Wizara ya mifugo wahakikishe wanasimamia mipango ya serikali kwa kusaidiana na viongozi wa chini ambao wanaonekana kuhemewa.”alisema Mkufya.
Nae mtendaji wa kijiji cha Kibindu ,Juma Mgaza ,alifafanua kuwa tukio hilo limetokea kweli,na wamesikitika kuona hali inatishia kuwa mbaya .
Alisema baada ya kutokea vurugu hizo waliwakimbiza hospitalini majeruhi ambapo Zaina alionekana kujeruhiwa vibaya kutokana na kuchomwa kisu cha titi.
Mgaza alisema chanzo cha mgogoro huo ni kufa kwa ng’ombe za wafugaji na kudai wamepewa sumu kwa makusudi.
Hali hiyo ilisababisha afisa mifugo wa kata ya Kibindu,John Fransis kupima mifugo hiyo na kubaini kuwa hakuna sumu waliyopewa kwa kukusudia zaidi ya kula majani aina ya kisamvu yanayobadilika kuwa sumu wakati wa ukuaji wake.
Mkazi wa kata ya Kibindu, Salum Ramadhani Mayue ,alisema anashukuru wao hawakupigwa ila walivamiwa na wafugaji ambako  walihakikisha wanawafukuza katika maeneo yao ya mashamba .
Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Boniventure Mushongi,alikiri kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia jan 10 na kusema uchunguzi unaendelea .
Alisema majeruhi walilazwa katika hospitali iliyopo mkoani Morogoro hivyo taarifa zaidi zinaendelea kufuatiliwa juu ya hali zao kutokana kulazwa nje ya mkoa wa Pwani.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,alisema suala  hilo linashughulikiwa na ofisi ya wilaya,polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine ili kubaini waliohusika na wachukuliwe hatua za  kisheria.
Alitoa rai kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kutii agizo la serikali ya mkoa kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo mkoani hapo.
Mhandisi Ndikilo,aliwasisitiza wakuu wa wilaya ,wakurugenzi ,maafisa tarafa mkoani hapo,kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka katika maeneo yao.
Mbunge wa jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete ,aliitaka jamii na viongozi kuanzia ngazi ya chini kushirikiana na serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoiungia kinyemela.

Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji jimboni humo ,Ridhiwani aliiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro hiyo.

Related Posts

Post a Comment