Waziri mkuu Kassim Majaliwa akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha Chai Lupembe alipotembelea kiwandani hapo.
SERIKALI imesema kuwa haita kubali kuendelea kusimamisha
viwanda kwa sababu wa migogoro baina ya viwanda hivyo na vyama vya ushirika kwa
maslahi ya watu wachache na kuwa viwanda vitaendelea kufanyakazi wakati
matatizo yakishighulikiwa na serikali.
Kauli hiyo inatolewa na waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim
Majaliwa ambayo ameitoa alipo tembelea kwenye kiwanda cha Chai ya Lupembe
mkoani Njombe ambacho kilisimama kwa muda na kusababisha miundombinu yake na
mali zake kudaiwa kuhujumiwa.
Waziri mkuu anaingia mkoani Njombe kwa mara ya pili ndani ya
mwenzi huu na kutembelea kiwanda cha Chai Lupembe na kusema kuwa serikali haita
kubari kiwanda kusimama kufanya kazi bali itahakikisha migororo inayosumua
viwanda hapa nchini.
Waziri Majaliwa anasema kuwa serikali itahakikisha inafufua
viwanda vilivyo fungwa kwa kushindwa kuendesha na kuhakikisha kuwa vipya navyo
vinafunguliwa ili watanzania kupata ajira humo.
Amesema kuwa watanzania waendelee kuzalisha malighafi na
zitafanyiwa uchakataji hapahapa nchini na kuhakikisha kuwa nchi za nje
zinachukua mali ambazo tayari zimesha ongezewa thamani.
Waziri mkuu baada ya kutembela kiwanda hicho anakutanana
wananchi wa kijiji cha Igombola ambapo
anasema kuwa wanakulima waendelee kulima chai na kupeleka kiwandani hapo kwa
kuwa hakita simama.
Pamoja na mambo mengine waziri majaliwa anasema kuwa matatizo
ya maji serikali itashughulikia mgogoro baina ya bodi ya maji inayo maliza
mdawake na iliyo po sasa kwa kumtua mkuu wa wilaya hiyo ya Njombe kufika kijijini
hapo kutatua tatizo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafili anasema kuwa serikali
itahakikisha kuwa wananchi wanapata maji bila kuwapo kwa vikwazi na Februari 2
mwaka huu kuingia katika kijiji hicho kukutana na viongozi ili kutoa suruhu.
Kuhusu umeme Shirika
la Umeme linasema kuwa tayari kijiji hicho kimetengewa Kipooza umeme na ngunzo
zinaanza kusimikwa wiki ijayo na kuanza kusambaza umeme majumani.
Post a Comment
Post a Comment