VIDEO: NDEGE YA ATCL ILIPOWASILI DODOMA KWA MARA KWANZA LEO


Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo limefanya safari yake ya kwanza kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Makao Makuu ya Tanzania, mkoani Dodoma.

Ndege iliyofanya safari hiyo ya leo asubuhi ambayo baadhi ya wabunge pia walikuwa wakielekea mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya kamati za bunge vinavyoanza leo, ilipokelewa kwa shangwe dodoma huku ikipewa saluti ya majini (water salute) katika uwanja wa ndege mjini Dodoma.

Mbunge wa Kigamboni, Faustine Engelbert Ndugulile (kushoto) akiwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe (kulia) walipokuwa wakielekea mkoani Dodoma kwa ndege ya ATCL leo pamoja na abiria wengine.

Shirika hilo linaendelea kuwasihi watanzania kuendelea kutumia ndege hizo kwa ajili ya safari mbalimbali ikiwemo Arusha, Kilimanjaro, Bukoba, Zanzibar, Mwanza ili kuliwezesha shirika hilo kukua zaidi na kuboresha huduma.

Video ya ndege ya ATCL ilipowasili uwanja wa ndege mjini Dodoma leo asubuhi.
NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA #TANZANIA (ATCL) IILIPOTUA KWENYE UWANJA WA NDEGE MKOANI DODOMA KWA MARA YA KWANZA.

Related Posts

Post a Comment