const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); SIMBA BADO MDEBWEDO KWA AZAM - HABARI MPYA

..

SIMBA BADO MDEBWEDO KWA AZAM

Ile ndoto mbaya ambayo mashabiki wa Simba walikuwa wanaomba dua isikatokee imeibuka jana baada ya kukubali kipigo cha goli 1 – 0 kutoka kwa Azam FC.

Awali, Simba walikuwa na kiburi cha kuongoza ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga.

Kwa kukubali kichapo hiki, Simba wamewapa nafasi kubwa wapinzani wao kwa kuongoza ligi hiyo yenye ushindani endapo Yanga itashinda mchezo wake utakaopigwa jioni ya leo dhidi ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga kuanzia saa kumi.

Ni wazi kabisa kuwa mashabiki wa Simba kwa sasa wamepata tumbo joto hasa kwakuwa wapinzani wao wana “advantage” ya kuongoza ligi na pia hata kuutetea ubingwa wao katika msimu huu.

Hii ni mara ya pili kwa Simba kupokea kipigo kutoka kwa Azam FC ndani ya wiki mbili tu za mwezi huu baada ya awali kupokea kichapo kama hicho kutoka kwa wana “lamba lamba”

Related Posts

Post a Comment