const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Sikihofii kivuli cha Mr T Touch – Producer mpya wa Free Nation ya Nay wa Mitego - HABARI MPYA

..

Sikihofii kivuli cha Mr T Touch – Producer mpya wa Free Nation ya Nay wa Mitego


Ukitaja orodha ya producers wakali na wanaofanya vizuri kwa sasa hapa Bongo, lazima Utamtaja Mr T Touch,mmiliki wa studio ya Touchez Sound iliyopo mitaa ya Sinza Jijini Dar es Salaam.

Nay wa Mitego akiwa na producer wake mpya, Ossam kwenye studio za Free Nation

Producer huyo ambaye amepika kibao za wakali kama Young Dee,Black Rhyno,Bill Nas na wengineo,alianza kuliteka soko kipindi anafanya kazi studio za Free Nation zinazomilikiwa na Nay wa mitego.

Sasa hivi Free Nation kuna producer mpya,anayefahamika kama Ossam, producer ambaye wengi wanaamini lazima ana kitete kufuta historia ya T Touch kwenye studio hiyo,suala ambalo kupitia Supermega ya Kings FM, Amedai ni kitu ambacho hakimpi shida.

“Suala la kusema kwamba kuna ugumu kisa alikuwepo Mr T, hamna,” Alisema. “kufanya tu kazi kali,naamini kila kitu kitaenda sawa,” amesema Ossam.

Related Posts

Post a Comment