Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Dudu Baya amedai ukimya wake kwenye muziki umesababishwa na kuwa busy kwenye biashara na siyo kwamba amefulia kama baadhi ya watu wanavyodai.
Rapper huyo amedai kwa sasa maisha yake yako Mwanza na Kampala akija Dar anakuja kufanya kazi za kisanaa japo alishaamua kupotezea muziki na kufanya biashara zake mbalimbali kwa kuwa haishi kwa kutegemea mziki pekee.
“Dudu Baya sijafulia kama watu wanavyodhani mimi na biashara zangu nyingine na muda mwingi sipo Dar es Salaam. Watanzania ndiyo tabia yao hiyo wakiona msanii haonekani wanadhani amefulia mfano watu walipoona King Crazy GK amepotea walidhani amefulia kumbe alikuwa chimbo anapiga kitabu na saizi tayari ana masters yake” Dudu Baya alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Pia Dudu amesema kauli ya Darasa kuimba kwamba ‘siyo chui, simba wala mamba ngozi yake inamtosha kujigamba’ haijamsumbua kwa kuwa Darasa ni kijana wake na ni msanii ambaye amepambana kwa muda mrefu ila kwa sasa kafanikiwa hivyo anampongeza kwa mafanikio
Post a Comment
Post a Comment