const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Serikali ya Swaziland yatoa agizo kwa shule kutoa elimu ya ukristo pekee - HABARI MPYA

..

Serikali ya Swaziland yatoa agizo kwa shule kutoa elimu ya ukristo pekee

Wizara ya elimu wiki iliopita iliwaagiza walimu wote wakuu kuhakikisha kwamba mtaala hautaji dini nyengine zaidi ya ile ya kikristo.

Wizara ya elimu wiki iliopita iliwaagiza walimu wote wakuu kuhakikisha kwamba mtaala hautaji dini nyengine zaidi ya ile ya kikristo.

Shule zimefunguliwa nchini Swaziland chini ya agizo jipya la serikali kufunza somo la dini ya kikristo pekee, hatua iliokosolewa kwa kuwa inakataa kuheshimu dini nyengine kulingana na chombo cha habari cha AFP.

Wizara ya elimu wiki iliopita iliwaagiza walimu wote wakuu kuhakikisha kwamba mtaala hautaji dini nyengine zaidi ya ile ya kikristo.

Kimemnukuu Sahid Matsebula, raia muislamu ambaye anafanya kazi msikitini karibu na mji mkuu wa Mbabane, kwamba sera hiyo huenda ikazua wasiwasi wa kidini katika ufalme huo.

“Serikali ina mpango gani kwa watoto wetu ambao sio Wakristo? Watafunzwa kitu kimoja nyumbani na kufunzwa kitu chengine shule,”.

Sera hiyo mpya inajiri baada ya raia kulalama kwamba wahamiaji wa bara Asia na wale wa kiislamu wamekuwa wakiingia nchini humo hatua iliolazimu bunge kubuni kamati ya kuchunguza mwaka uliopita, AFP imeripoti.

Related Posts

Post a Comment