Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya FIFA
Ronaldo, 31, amewapiku Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Ronaldo pia alishinda tuzo ya Ballon d’Or mwezi Disemba mwaka jana, kufuatia mafanikio yake katika Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, na pia kushinda Euro 2016 akiwa na timu ya taifa ya Ureno.
Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri ametajwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, huku Silvia Neid, meneja wa zamani wa Ujerumani, akishinda kwa upande wa wanawake.
Post a Comment
Post a Comment