Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama amekosoa amri iliyosainiwa na Rais Trump ya kuzuia wahamiaji kutoka nchi saba na kuzuia wakimbizi kuingia Marekani kwa siku 90.
Rais Obama ambaye ametoka madarakani siku 10 zilizopita amesema kupitia kwa msemaji wake, Kevin Lewis kuwa si sahihi kubagua watu kwa minajili ya imani zao.
Aidha katika taarifa hiyo iliyotolewa jana Jumatatu, Rais Obama ameunga mkono maandamano yanayayoendelea maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kwenye viwanja vya ndege wakipinga kuzuiwa kwa wahamiaji na wakimbizi kuingia Marekani. Waandamanaji wanadai kuwa Marekani ni taifa la mchanganyiko wa watu kutoka maeneo mbalimbali hivyo zuio hilo si halali.
Lewis alisema kuwa Rais Obama amesema kuwa maandamano hayo yanayonyesha kile kinachotokea endapo taratibu na kanuni za Marekani zinavunjwa.
Aidha, taarifa hiyo imekaata kufananisha zuio lililowekwa mwaka 2011 na Rais Obama ambapo raia wa Iraq walizuiwa kuingia Marekani baada ya kule kilichoelezwa kuwa kuna raia wawili walioomba hifadhi Marekani walikula njama za kutaka kufanya ugaidi na zuio la Trump la wakimbizi na wahamiaji toka nchi saba pamoja na ujenzi wa ukuta.
Rais Trump amenukuliwa akisema kuwa zuio la nchi saba ametekeleza kama matokeo ya uamuzi uliofanywa na Rais Obama mwaka 2011 ambapo katika ripoti aliziorodhesha nchi hizo kama tishio kwa usalama wa Marekani.
Post a Comment
Post a Comment