const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); PICHA: TRENI YA DAR ES SALAAM- KIGOMA YAPATA AJALI MKOANI PWANI - HABARI MPYA

..

PICHA: TRENI YA DAR ES SALAAM- KIGOMA YAPATA AJALI MKOANI PWANI


Gari Moshi linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Kigoma limepata ajali mkoani Pwani leo alasiri. Taarifa za awali zinaeleza kuwa gari moshi hili limepata ajali umbali mdogo kutoka kilipo kituo chake (stesheni) ya Ruvu.

Taarifa kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRL) zinaeleza kuwa treni hiyo ya Deluxe kutoka Kigoma imepata ajali saa 9:45 alasiri leo kati ya stesheni za Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa mawili yameanguka na mengine matatu yameacha reli.

Taarifa za majeruhi katika ajali hiyo hazijakamilika lakini Gadi ameripoti mtu mmoja yuko mahututi huku wengine wakiwa na majeraha madogo madogo mwili mwao.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alikuwa njiani kuelekea eneo la tukio akiwa ameambatanana na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Masanja Kadogosa, Kamanda wa Polisi (RPC) Chilery na Kikosi cha Uokoaji cha TRL. Kikos cha uokoaji kupo na crane ya kunyanyulia mabehewa.


Tunafuatilia kwa karibu tukio hili tutaendelea kukukjuza, endelea kuwa nasi.

Related Posts

Post a Comment