Picha: Mwili wa Mwandishi wa Habari aliyefia Zanzibar Ukisafirishwa kwenda Dar


Mwili wa mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la uhuru na mzalendo Amina Athuman ukisafirishwa asubuhi hii na boti ya kilimanjaro kuelekea Dar es Salaam na kusafirishwa hadi kijijini kwao Lushoto kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumanne mchana. Marehemu alikuwa Zanzibar kikazi akiripoti habari za michezo kombe la Mapinduzi na kumkuta mauti hayo baada ya kujifungua mtoto wa kiume, kwa bahati mbaya mtoto akafariki baada ya kuzaliwa na yeye kupata kifafa cha uzazi na kufariki jana asubuhi. Mwenyenzi mungu ampe kauli thabiti na amsamehe madhambi yake-Ameen

Related Posts

Post a Comment