const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Pengine Apple Ikazalisha iPhone X 2017! - HABARI MPYA

..

Pengine Apple Ikazalisha iPhone X 2017!


Apple naweza kusema kuwa ndio kampuni linaloongoza duniani kwa kuleta simu bora na zenye ubunifu wa hali ya juu kulingana na ripoti zilizopo.

Japokuwa wengine wanasema kampuni imejipatia mafanikio makubwa sana katika simu zake za iPhone 6 na 7 baada ya kampuni ya Samsung kupata majanga juu ya simu zake za Samsung Gallaxy Note 7.Simu aina ya Samsung Galaxy Note 7 ilyolipuka.

Simu hizo zilikuwa na athari katika sehemu yake ya betri hali ambayo ilisababisha simu hizo kulipuka. Tuachane na Samsung kidogo turudi kwa Apple

Kampuni inasemekana ipo katika utangenezaji wa iPhone ambayo inaweza ikawashangaza watu kama lile toleo la mara ya kwanza lilivyoshangaza wengi (iPhone SE).Apple

Toleo hili linasemekana kuwa litaitwa iPhone X na kuna uwezekano mkubwa kuwa linaweza likatoka na simu za iPhone 8

Jina la iPhone X limewaacha watu midomo wazi wakati wengi wao wanaisubiria kwa hamu sana ili kujionea kuwa ni kitu gani itakuwa imekibeba. Pengine mwaka huu inaweza isitoke iPhone 8 na ile X ikawa ndio mbadala au zikatoka zote kwa wakati mmoja.

Vile vile kwa kuwa kampuni inatimiza miaka kumi tangia ianze kutengeneza simu janja za iPhone jina la simu hii yaani iPhone X linaweza likawa linasimama baada ya tukio hilo

Cha kuangalia pia ni kwamba X ni namba ya kirumi ambayo inamaanisha 10 hivyo hii pia inaweza ikawa ni sababu

Inasemekana kuwa kampuni inaweza ikaongeza mambo mengi sana katika simu hii ikiwemo na uwezo wa kutambua sura (facial recognition) badala ya utambulizi wa vidole (finger print)Apple

Kaa karibu na TeknoKona kwani uhakika zaidi ukipatikana, utakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa kupitia mtandao wako pendwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, hili umelipokeaje? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Related Posts

Post a Comment