Mwimbaji wa nyimbo za Injili jijini Mbeya, Aman Mwasote
Mwimbaji wa nyimbo za Injili jijini Mbeya, Aman Mwasote (kulia), akiwa na wakili wake, Sambwee Shitamba anayemtetea katika kesi ya kutuhumiwa kumwita mchawi mtoto wa kike (9) jina linahifadhiwa wakati akiwa kwenye mkutano wa injili wakiwa nje ya Mahakama ya Wilaya Mbeya.
MWIMBAJI wa nyimbo za Injili jijini Mbeya, Aman Mwasote amepandishwa kizimbani akituhumiwa kumwita mchawi mtoto wa kike wa miaka 9 jina linahifadhiwa wakati akiwa kwenye mkutano wa injili.
Kesi hiyo yenye namba CC 168 inayomkabili Mwinjilisti na Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Amani Mwasote imeendelea kusikilizwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya.
Mwendesha mashtaka wa Serikali katika kesi hiyo Heberi Kihaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Venance Mlingi alidai kuwa Septemba 20,2016 mwimbaji huyo akiwa kwenye mkutano wa injili alimtuhumu binti huyo kuwa ni mcahawi.
Kihaka alisema kulingana na shtaka hilo upelelezi ulikamilika na wako tayari kuleta mashahidi ambapo Mahakama ilimuona Amani ana kesi ya kujibu.
Aidha mshtakiwa huyo ambaye alikuwa akisimamiwa na wakili wa utetezi Sambwee Shitambala alitakiwa kuanza kujitetea.
Akimuongoza mtuhumiwa Amani Mwasote alikanusha kumwita mtoto huyo ni mchawi bali mtoto huyo alikumbwa na pepo hivyo alifika katika mkutano huo kwa maombezi kama walivyofanya watu mbalimbali wakubwa kwa wadogo.
Upande wa utetezi ulileta mashahidi wawili ambao ni walimu wa Amani Mwasote katika chuo cha Biblia Kalobe.
Baada ya mashahidi hao upande wa utetezi kumaliza utetezi na upande wa mashitaka Hakimu Venance Mlingi aliahirisha kesi hadi February 6 mwaka huu mahakama itakapotoa hukumu.
Mlingi alisema dhamana kwa mtuhumiwa inaendelea hadi siku itakayotolewa hukumu.
Post a Comment
Post a Comment