const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Mwenyekiti wa Kijiji afariki baada ya kusikia mchungaji wake kafa kwa Ajali - HABARI MPYA

..

Mwenyekiti wa Kijiji afariki baada ya kusikia mchungaji wake kafa kwa Ajali



mwenyekiti wa kijiji cha Mkiu katika kata ya Lubonde wilayani Ludewa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw.Kretus mtewele Amefariki Dunia Usiku wa kuamkia Leo January 25 katika hospital ya misheni Lugarawa.

Taarifa kutoka kwa diwani wa kata hiyo Mh. Nicholaus Mgaya (CCM) zinasema kuwa Marehemu Alipatwa na mshtuko mkali baada ya kupokea Taarifa za Kifo cha mchungaji Frenk Ngatunga wa kanisa Anglican mtaa wa kiyombo aliyefariki kwaajali ya Pikipiki iliyotokea January 22 mchana mwaka huu huko katika kijiji cha mkiu Barabara ya kuelekea Kiyombo.
Mh Mgaya amesema kuwa Anafanya kikao kidogo cha mazungumzo na watumishi wa kata yake asubuhi hii ili kuweza kukamilisha taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu pamoja na Taratibu za Mazishi.

Related Posts

Post a Comment