Mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la JAPHET amekamatwa na kikosi maalum kinachohusisha TRA , POLISI na MAAFISA WA KILIMO akiwa anavusha mahidi kwa njia ya panya kutoka nchini Malawi bila ya kufuata utaratibu wa sheria.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 4:30 asubuhi, katika mpaka wa nchi ya Malawi na Tanzania wa Kasumulo Wilayani Kyela, kinyume na sheria za uingizaji chakula nchini.
Mahidi hayo yamekamatwa yakiwa kwenye gari moja aina ya Canter na mengine yalikuwa yamehifadhiwa kwenye 'store'.
Wakati wa uchukuaji wa mahidi 'store' kundi la wananchi walijitokeza na walianza kuwazuia maafisa wa TRA kupakia mahindi hayo kwa kile walichodai kuwa wanauziwa mahindi hayo kwa bei rahisi.
Kutokana na hali hiyo Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao na baadaye hali kurejea kuwa shwari
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema linaendelea na ufuatiliaji wa karibu ili kubaini wafanyabiashara wenye tabia kama hiyo.
Post a Comment
Post a Comment