Klabu ya soka ya Manchester United imetengeneza pesa zaidi ya klabu yoyote ile duniani katika msimu uliopita, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Deloitte.
Waliotolewa kwenye nafasi hiyo ni Real Madrid ya Hispania – ambao wamekuwa vinara wa list hiyo kwa miaka 11 – baada ya kukusanya kiasi cha “Yuro” milioni 689 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania trilioni moja na bilioni mia sita thelathini na nane katika msimu wa 2015-16.
Hii ni mara ya kwanza kwa ‘Man U’ kuongoza katika ripoti hiyo inayotolewa kila mwaka na kujulikana kama “Deloitte Football Money League” tangu msimu wa 2003-04.
Real Madrid inashuka mpaka nafasi ya tatu, nyuma ya mahasimu wao Barcelona, ambao bado wanaendelea kushika nafasi ya pili.
Miamba ya Ujerumani, klabu ya Bayern Munich imepanda mpaka nafasi ya nne na Man City pia imepanda mpaka namba tano kutokana na pesa ambazo klabu hizi zimetengeneza katika msimu uliopita wa ligi. Hii ni mara ya kwanza kwa City kufika nafasi ya tano katika ripoti hii ya mwaka.
Leicester City wanaoshika nafasi ya 20 wameingia kwenye 20 bora kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo. Klabu za Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham zinabaki katika nafasi zake za awali za saba, nane, tisa na 12, na West Ham katika nafasi ya 18.
Orodha ya klabu 10 za juu ni kama ifuatavyo:
“Deloitte Money League Table 2015-16” | ||
---|---|---|
Timu (msimu uliopita) | Mapato (Dola milioni) 2015-16 | Msimu wa 2014-15 |
1 (3) Manchester United | 734.2 | 554.1 |
2 (2) Barcelona | 660.9 | 598.1 |
3 (1) Real Madrid | 661.1 | 615.2 |
4 (5) Bayern Munich | 630.9 | 505.5 |
5 (6) Manchester City | 559.6 | 494.1 |
6 (4) Paris St-Germain | 555.3 | 512.7 |
7 (7) Arsenal | 499.5 | 464.3 |
8 (8) Chelsea | 476.9 | 447.7 |
9 (9) Liverpool | 430.5 | 417.7 |
10 (10) Juventus | 363.7 | 345.3 |
Post a Comment
Post a Comment