Mwaka 1993 mwezi March Mpiga picha maarufu wa Africa kusini (PhotoJournalist) Kevin Carter alitembelea Nchi ya Sudan kwa ajili ya kupiga picha za habari kuhusiana na baa la njaa lililoikabili nchi hiyo.
Ni kipindi ambacho nchi ya Sudan ilikumbwa na baa kubwa sana la njaa hali iliyopelekea watu wengi kufa njaa na wengine wakihangaika kuokoa uhai wao kwa kula Magome ya miti, nyasi na mizizi.
Ni kipindi kibaya sana katika Historia ya Sudan kwa sababu Jumuiya ya kimataifa ilisita kupeleka msaada wa chakula kutokana na hali mbaya ya kisiasa iliyokuwepo Sudan (vita vya wenyewe kwa wenyewe).
Japo baadae umoja wa Mataifa (UN) ulikubali kupeleka msaada wa Chakula lakini watu wengi walikua wameshapoteza maisha kutokana na baa la njaa.
Ni kipindi hiki ndipo Kevin Carter alienda nchini Sudan akifuatana na Mwandishi mwenzie wa kireno João Silva kuripoti juu ya baa la njaa lililoikumba nchi hiyo.
Katika kutekeleza wajibu wake wa kikazi Kevin alifanikiwa kupiga picha ya mtoto mmoja mdogo aliyeshindwa kuendelea na safari ya kuwafuata walezi wake waliokuwa wameenda kupokea chakula cha msaada toka UN. Mtoto huyo alipewa jina la Ken.
Ndege za UN zilikua zikidondosha msaada wa chakula kwa wanakijiji wa eneo hilo. Wazazi wa Ken walifariki kwa njaa na yeye kulelewa na jamaa wa karibu.
Siku hiyo walezi wa Ken walienda kuokota chakula cha msaada kilichokuwa kikidondoshwa na ndege za UN. Ken alijaribu kuwafuata walezi wake lakini aliishindwa kuendelea na safari katikali ya pori kutokana na uchovu, njaa kali, kiu, na mwili kukosa nguvu. Akiwa peke yake porini alianguka.
Akajaribu kuficha kichwa chake ardhini kutokana na jua kali lililokua likiwaka (zaidi ya nyuzijoto 40°C). Hapakuwa na mti wa kujikinga maana miti ilikauka kwa ukame, mingine watu walikula magome wakiwa katika jitihada za kujiokoa na njaa.
Ken hakujua kuwa nyuma yake kulikua na ndege aina ya "tai" ambaye hula mizoga na alikua akimnyemelea. Akiwa pale chini alivamiwa na ndege huyo ambsye alimdonoa sehemu ya utosi na kumuua kabla ya kuanza kula nyama yake kwa kudonoa kama adonoavyo mizoga.
Wakati Ndege huyo akimkaribia Ken, mwandishi wa Habari Kevin Carter alikua na Camera yake akipiga picha. Baadae akachukuliwa na ndege za UN na kumuacha mtoto huyo akiliwa na "tai" bila msaada wowote.
Picha hiyo ilichapishwa kwenye gazeti la New York Times tar.26 March 1993 na kuibua mjadala mkubwa juu ya maadili ya taaluma ya upigaji picha za habari (Ethics of Photojournalism).
Wengi walilaumu kitendo cha Kevin Carter kupiga picha na kuacha kuokoa maisha ya mtoto yule. Katika utetezi wake Carter alisema hakujua kama tai yule angemshambulia Ken.
Aliongeza kuwa alisubiri kwa muda wa dakika 20 kuona kama tai yule angerusha mbawa zake kumsogelea Ken. Alipoona tai huyo hamsogelei mtoto huyo aliamua kuondoka kwa ndege maalum za UN zilizokua zikitoa msaada eneo hilo na kumuacha mtoto Ken peke yake. Lakini baadae akaambiwa kuwa mtoto huyo alidonolewa na tai hadi kufa.
Taarifa nyingine zinadai kuwa Carter alikua akitekeleza kazi aliyopewa na muajiri wake, kwamba akifika Sudan afanye kazi moja tu ya kupiga picha na alizuiwa kufanya kazi ya uokoaji kwa sababu hakwenda Sudan kwa kazi hiyo.
Pamoja na hayo yote Carter alitunukiwa tuzo kwa Picha hii, mnamo mwezi April mwaka 1994 kwenye tuzo maarufu za Pulitzer. Picha hii ilipewa tuzo ya kuwa picha bora ya makala (Feature Phoyograph).
Lakini Carter hakuifurahia tuzo hiyo kutokana na kukosa utu ambao ulipelekea kifo cha mtoto Ken. Aliishi maisha ya masononeko na kujilaumu kila mara kwa kushindwa kuokoa maisha ya mtoto yule.
Aliomba radhi kwa kusema ''kwakweli naomba msamaha kwa kutomuondoa mtoto huyo katika mazingira ya hatari (“I’m really, really sorry I didn’t pick the child up,”).
Tar.27 mwezi July mwaka 1994 (miezi minne tu baada ya kupokea tuzo) Kevin Carter aliamua kujiua kwa sumu ya Carbon Monoxide (Carbon monoxide poisoning) kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na historia ya Sudan ya kifo cha mtoto Ken.
Kevin Carter alilipwa fedha nyingi sana na gazeti la New York Times kwa picha ile. Hali kadhalika alipewa tuzo ya heshima kwa upigaji picha bora, lakini baadae akaona vyote havina thamani kwa kitendo alichokifanya kwa kukosa utu.
Kabla ya kujiua Carter aliandika ujumbe kwenye kipande cha karatasi akisema "Maumivu ya moyo yanazidi furaha ya fedha" (The pain of heart overweigh the joy of getting money)...
.... Najisikia vibaya sana, kumbukumbu za mauaji, njaa na mateso ya mtoto Ken zinanijia kila mara. Naenda kumfuata na kumuomba msamaha kama nitapata bahati ya kufanya hivyo... ( I am so depressed ... I am haunted by the vivid memories of killing, anger and pain of starving child Ken... I have gone to join him and ask for forgiveness if that opportunity arrise.
Post a Comment
Post a Comment