Kauli ya Katibu Tawala Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Robert Siyantemi imezua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya kunukuliwa akishauri kuwa tafiti za kisayansi zifanyike ili kuona uwezekano wa kutumia damu za wanyama kwa binadamu.
DAS Robert Siyantemi alitoa ushauri huo alipokuwa kwenye mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Arusha, mkutano uliofanyika wilayani Arumeru chini ya Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo.
Siyantemi alishauri hivyo kutokana na changamoto kubwa inayoikabili Wizara ya Afya katika kuijihakikishia upatikanaji wa damu salama na ya kutosha kwa ajili ya wagonjwa mahospitalini. Siyantemi alisema kutokana na uwepo wa changamoto kuwa ya kuhakikisha usalama wa damu, ni bora uangaliwe utaratibu wa kutumia damu za wanyama.
“Mheshimiwa mwenyekiti naamini utafiti umeshafanyika au unaendelea kufanyika, nashauri damu za wanyama hasa hawa wanaofanania na binadamu kama nyani, tumbili na kima damu zao zifanyiwe utafiti tuone kama zinaweza kutusaidia,” alisema
Siyantemi alikua miongoni mwa wanachama 42 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotia nia wakitafuta kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Mtia nia huyu alijizolea umaarufu akiwa mtia nia kijana kuliko wote.
Post a Comment
Post a Comment