Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limepiga marufuku kuanzia hivi sasa kufunga ndoa madhabahuni kwa wanawake waliozaa.
Aidha, limepiga marufuku pia ufungishaji wa ndoa madhabahuni kwa wanawake wajawazito kwa maelezo kuwa kufanya hivyo ni kukiuka maagizo ya na maandiko ya Mungu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika gazeti la Nipashe la leo Jumapili Januari 22, 2017 wanawake wenye sifa hizo hawataruhusiwa kusimama mbele ya madhabahu na kufunga ndoa wakiwa wamevaa shela.
Utaratibu mpya uliotangazwa na kanisa hilo kuwafungisha ndoa waumini wenye sifa hizi ni kuwa watafungishwa wakiwa katika ibada ya kawaida wakiwa wamekaa na waumini wengine.
Kanisa hilo limesema kuwa wanawake wenye watoto au wajawazito watatakiwa kubariki ndoa zao bila kuvaa shela jeupe. Hivyo kitaachokuwa kinafanyika sio kufungisha ndoa badala yake ni kubariki ndoa.
Mmonye wa maofisa wa Makao Makuu ya KKT alieleza gazeti la Nipashe kuwa lengo kubwa la tangazo hilo lililosomwa katika makanisa mengi juma lilikuwa kuwakumbusha waumini kurudi katika sheria za Mungu ambazo zinataka mwanamke aliyezaa kabla ya kufunga ndoa au mjamzito arudi kundini kwanza kisha abariki ndoa.
Akizungumzia suala la uvaaji shela, afisa huyo alisema kuwa shela nyeupe hutakiwa kuvaliwa na wanandoa ambao hawajawahi kukutana kimwili.
Post a Comment
Post a Comment