Kalapina ambaye ni mwanaharakati aliyejikita katika kupambana na kuwasaidia watu mbalimbali walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya amezungumzia suala la msaani Rashid Mkwiro maarufu Chid Benz la kuzama kwenye matumizi ya dawa na kusema kuwa chanzo kikubwa na mama yake.
Kutoka kushoto ni Babu Tale, Kalapina na Chid Benz.
Kalapina amesema kuwa mama yake Chid Benz amekuwa akimdekeza mtoto wake kiasi cha kumfanya ashindwe kuacha kutumia dawa za kulevya. Alieleza kuwa Chid Benz anadekezwa kiasi cha kujua kwamba hata akifanya jambo baya kiasi gani mama yake atakuwa upande wake na kumtetea.
Kalapina alisema hayo jana kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha runinga cha EATV na kusema kuwa zamani masuala haya hayakuwa yameshamiri sababu mtoto alikuwa akifanya kitu cha kijinga, basi kipigo kinaanzia nyumbani na hivyo atanyooka tu.
“Kiukweli mama yake mzazi Chid Benz anampenda sana mwanaye na hali hiyo inampelekea mdogo wangu yule kuona hata nikizingua mama atanitafuta tu, au kuona mama atasimama na yeye tu sababu mama yake anampenda sana, lakini siyo Chid Benz tu wazazi wengi wanawalea watoto kwa kuwadekeza sana, wazazi hawana muda na watoto na hili linachangia vijana kuingia kwenye madawa ya kulevya hata kwenye ushoga pia, lakini sisi wazazi wetu zamani ulikuwa ukizingua unapigwa sana hivyo lazima utanyooka tu” alisema Kalapina
Post a Comment
Post a Comment