Rapper Kalapina ambaye amekuwa mstari wa mbele kusaidia baadhi ya watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya amemtaja mtu ambaye anasababisha Chidi Benz asiachanwe na matumizi hayo.
Kalapina amemtaja mama yake mzazi Chidi ndio anayesababisha rapper huyo asiachane na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa amekuwa akimdekeza sana.
“Kiukweli mama yake mzazi ChidI Benz anampenda sana mwanaye na hali hiyo inampelekea mdogo wangu yule kuona hata nikizingua mama atanitafuta tu, au kuona mama atasimama na yeye tu sababu mama yake anampenda sana,” Kalapina amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
“Siyo Chidi Benz tu wazazi wengi wanawalea watoto kwa kuwadekeza sana. Wazazi hawana muda na watoto na hili linachangia vijana kuingia kwenye madawa ya kulevya hata kwenye ushoga pia. Lakini sisi wazazi wetu zamani ulikuwa ukizingua unapigwa sana hivyo lazima utanyooka tu,” ameongeza.
Post a Comment
Post a Comment