Kikosi cha Yanga
Kuelekea mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar kati ya Simba na Yanga, mshambuliaji wa Simba Juma Luizio, amekubali makali ya kikosi cha Yanga na kusema kuwa kinaundwa na wachezaji wazuri.
Luizio ambaye amesajili Msimbazi kwa mkopo akitokea Zesco ya Zambia licha ywa kukubali uwezo wa wachezaji wa Yanga, amesema kuwa hakuna anayemuogopa, na kwamba yuko tayari kwa pambano la kesho na atahakikisha anapambana kuipa Simba ushindi.
"Yanga ina wachezaji wazuri sana, wachezaji wote ni wazuri, lakini hakuna ninayemuhofia" Alisema LUizio mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Simba na Jang'ombe Boys, ambapo Simba ilishinda 2-0.
Akiwa Zesco ya Zambia, Luizio alikuwa akinolewa na kocha wa Yanga kwa sasa, George Lwandamina.
Juma Luizio akiwa Zesco
Katika michuano hii Luizio amefungia Simba bao moja pekee, alilofunga katika mchezo dhidi ya Taifa Jang'ombe huku akijihakikishia nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza.
Mechi hiyo inapigwa kesho saa 2;15 usiku katika dimba la Amaan, visiwani Zanzibar
Post a Comment
Post a Comment