Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.
Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.
Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.
Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. Nakumbuka nilikuwa naendesha baskeli kuelekea shuleni kupitia makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbali bmali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.
John Okello hakuwa na majibu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.
Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi.Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.
Viongozi wa A.S.P walifadhaishwa na matendo ya Okello (wengi wao, walikuwa hata hawapo visiwani wakati huo).Walikimbilia haraka kuwaunga mkono waasi. Mamia ya wafuasi wa vyama walipigwa na butwaa juu ya wale ambao walikuwa na shuku ya kukata fundo hilo gumu la majadaliano ya kidemokrasia na kukimbilia moja kwa moja kwenye utawala. Hawawalitafuta njia ya kuiandaa jamii kwenda sambamba na kanuni zao. Kanuni siku hizo zilikuwa ni ghali sana kama sarafu ya Marekani. Ubinadamu ulikuwa ni kitu adimu sana.
Baadhi ya viongozi wa ASP baada kuona kwamba serikali itakuwa haina udhibiti na uwezo kujilinda na kutokuwa na imani matokeo ya chaguzi huria zilizofanyika, viongozi hawalitafuta njia za haraka za kuhalalisha udhibiti yale ambayo yaliitwa sasa “Mapinduzi”. Makundi ya watu wenye fujo yalikuwa huru. Sheria na amani zilikuwa hazipo katika mitaa ya Zanzibar.
Walimiliki ardhi na wafanya biashara waliburutwa kutoka majumbani na madukani mwao, uporaji na mauaji yalienea mji mkongwe mzima. Kwa kweli mji wenyewe uliporwa.
Waarabu na Waasia , waliokuwa wakiunga mkono vyama vyengine waliuliwa kwa makundi. Kwa usiku mmoja maisha ya watu yasiyovika yalipotea na siku nyengine baadae maelfu ya watu waliikimbia nchi pamoja na kila walichoweza kubeba.
John Okello mwenyewe alijipachika cheo cha Jemedari Mkuu akishirikiana na bataliani zake zenye fujo walianzisha utawala wa vitisho ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba. John Okello alitangaza vitisho visivyo vya kawaida na ahadi ya kifo kwa wote watakaojaribu kumpinga yeye. John Okello aliamini alikuwa akipokea maelekezo /dokezo kutoka kwa Mungu na akionyesha uwezo usiokuwa wa kawaida kwa kutumia nambari, kwa mfano tarehe 13 Januari, 1964, alitangaza ujumbe ufuatao.” Serikali sasa inaendeshwa na sisi ikiwa mtakuwa wakaidi na kukataa kutii amri, Nitachukua hatua kali mara 88 zaidi ya hatua ninazozichukua hivi sasa” na “Na ikiwa yeyote atashidnwa kutii amri ya kutotoka nje ya nyumba kama walivyofanya wengine.sitokuwa na njia nyengine lakini kutumia silaha nzito.Sisi, ni jeshi lenye nguvu ya 99,099,000″.
Vitisho vyake na uwezo wake wa kuvitekeleza viliwatia hofu raia, hasa makundi mbali mbali ya jamii zilizo ndogo. Tarehe 14 Januari, 1964 alitangaza maneno haya ya kufadhaisha” Huyu hapa ni Jemedari Mkuu wa Unguja na Pemba Nafikiria kuelekea kijiji cha Mtendeni kukiangamiza ikiwa watu wa hapo hawatafuata amri. Baada ya dakika 40 nitawamaliza nyote hasa Wangazija”, ” na kwa vijana wote wa kiarabu wanaoishi Malindi; Nitapita Malindi nikiwa nimesheheni silaha ambazo mimi mwenyewe ndie nizijuazo. Nataka kuona kila mmoja abakie na chupi na kulala chini. Nataka kuwaona wao wanaimba… Baba wa Waafrika. Mungu Mbariki yeye na malengo yake na yale ya Jemedari Mkuu”
Wakati unyanyasaji uliposima jamii za tamaduni tofauti za Zanzibar zilikuwa zimeparaganyika. Taifa la chama kimoja lilitangazwa. Lakini bado jTaifa hili likihofia uwezekano wa kufufuka upinzani kutoka kwa wapinzani waliokimbia nchi.Wanamapinduzi hawa baadae walijihakikishia udhibiti zaidi baada ya kusaini mkataba wa muungano wa Tanganyika. Hii ingeruhusu maelfu ya marafiki wa kisiasa wa Tanganyika kuingilia kati upinzani wowote wa baadae katika visiwa hivi. Askari polisi wa Zanzibar walibadilishwa kwa askari polisi kutoka Tanganyika ambao ni watiifu kwa chama na pazia la siasa za utengano ziliwakumba wazanzibari ambazo zilitakiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 20.
Leo hii siasa hizi za utengano hazipo tena, kumalizika kwa vita vya baridi na kuelekea kwa uchumi wa kisasa umeweza kuifungulia Zanzibar milango kwa ulimwengu wa nje. Uchaguzi wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na mwengine unatarajiwa kufanyika mwaka, 2000. Viongozi wa kweli na wenye kujali hali za watu wameibuka Tanzania na hii imewafanya wakimbizi waliokimbia wakati wa mapinduzi kurejea visiwani. Uvumilivu na amani wa watu wa aina tofauti, ambayo ni tabia ya maisha ya wazanzibari, sasa hivi unajitahidi kurejea katika mitaa ya mji mkongwe.
Baadhi ya picha za watu waliotajwa katika historia hii ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Post a Comment
Post a Comment