Rapper mkongwe nchini Tanzania King Crazy GK, ameshauri serikali kuwachukulia hatua kali watu wanaotumia dawa za kulevya nchini.
“Marekani hawahudumiagi mtu mwenye madawa ya kulevya hata angekuwa anagalagala barabarani pale mpaka mwenyewe akajisahihishe na mgonjwa mwingine anahudumiwa bure kabisa,” rapper huyo amemuambia mtangazaji wa Ice Fm, Gami Deetz
Alipoulizwa iwapo ni sawa kuwaacha wafe, GK hakupepesa macho. “Enhee kwa mfano China wananyonga ina maana hawawapendi wananchi wao?”
Pia GK amemshauri Rais Dkt John Magufuli kulivalia njuga suala hili kutokana na umakini na utendaji wake wa kazi.
Kwa upande mwingine, GK amesema wasanii wengi huingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya kutokana na kutegemea muziki peke yake na pindi wanapochuja huwa na frustration za maisha na hivyo kujiliwaza kwa unga. Ameshauri wasanii waende shule ili kuwa na kitu cha kufanya pale muziki unapogoma
Post a Comment
Post a Comment