const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Bodaboda zagongana uso kwa uso Ludewa na kusababisha vifo - HABARI MPYA

..

Bodaboda zagongana uso kwa uso Ludewa na kusababisha vifo

Watu wawili wamefariki Dunia papo hapo katika ajali ya pikipiki kugongana uso kwa uso iliyotokea Hapo january 22 siku ya jumatatu mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kijiji cha Mkiu kilichopo Kata ya Lubonde wilayani ludewa Mkoa wa Njombe Katika Barabara ya kuelekea kijiji cha Kiyombo.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo akiwa ofisini kwake mkuu wa polisi wilaya ya Ludewa Emmanuel Gariyamoshi amesema kuwa waliofariki katika ajali hiyo ni Dereva bodaboda Aliyejulikana kwa Jina la Elipago Spriani Mpangwa na mkazi wa Kijiji cha Kiyombo wilayani Ludewa aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili Mc 971ACA aina ya Kinglion pamoja na abiria wake aliyejulikana kwa jina la Frenck Ngatunga mwenye umri wa miaka 45 mmanda na alikuwa mchungaji wa kanisa Anglican mtaa wa Kiyombo.

Ameongeza kuwa pikipiki hiyo waliyokuwa wakiitumia marehemu hao wawili iligongana uso kwa uso na pikipiki yenye namba za usajili MC 909 ADL Kinglion iliyokuwa ikiendeshwa na Moris Msemwa mwenyeumri wa miaka 35 Mpangwa na mkulima wa kijiji cha mkiu ambae ni majeruhi na baada ya ajali hiyo kutokea Huko katika Barabara ya Mkiu kuelekea kiyombo majeruhi alikimbizwa katika hospital ya misheni Lugarawa kwaajili ya matibabu.
Kamanda huyo Wa Jeshi la polisi wilaya ya Ludewa amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa madereva wa pikipiki zote mbili zilizogongana uso kwa uso Huku akisema kuwa baada ya kufanya uchunguzi miili ya marehemu wamekabidhiwa ndugu kwaajili ya taratibu za mazishi na hali ya Majeruhi aliyekimbizwa hospital inaelezwa kuwa inaendelea vizuri.
Hatahivyo Kamanda Gariyamoshi anatoa wito kwa waendesha pikipiki na madereva wote wa vyombo vya moto wilayani Ludewa kuendesha vyombo vyao kwakufuata Sheria za usalama barabarani ikiwemo kupunguza mwendo pindi wanapoendesha vyombo vyao.
Kwa mujibu wa Maelezo ya Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mkiu Bw. Leo Mlelwa pamoja na Diwani wa kata ya Lubonde Mh. Nicholaus Mgaya walipofanya mahojiano kwa njia ya simu na mwanahabari Maiko Luoga wanasema kuwa Mchungaji huyo wa kanisa Anglican Padre Frenk Ngatunga alikuwa akitoka kuendesha misa ya jumapili eneo la Lubonde hivyo alikutwa na ajali hiyo mbayaya iliyotoa uhai wake wakati akirejea nyumbani kwake Kiyombo.

Related Posts

Post a Comment