mtoto huyo (19) akiwa amekaa kwenye mkeka akiongea na waandishi wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akimpa pole mtoto huyo
Nyumba alipokuwa anaishi Sikujua Pesambili
Tuma Kitaba Msamaria mwema anaemtunza kwa sasa binti huyo
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akiongea na wanakijiji cha kiwanja kata ya mbugani wilayani Chunya
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya Chunya
MWANAUME mmoja alijulikana kwa jina la Maneno Pesambili Kanjanja (anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Chunya akituhumiwa kumfanya binti yake wa kumzaa kuwa mke ili hali ni mlemavu wa miguu kumnyanyasa.
Mwanaume huyo ambaye haelewani na majirani kutokana na ukali na alikamatawa Januari, 22 mwaka huu majira ya saa mbili usiku kitongoji cha mwakambonja kijiji cha kiwanja kata ya mbugani hapa.
Kwa mujibu wa majirani wa Mtuhumiwa huyo walisema walimuona binti huyo (19)akiwa anatambaa ya saa moja akitokea katika nyumba yao na kuelelea katika ghofu nyumba iliyopo mita 100.
Walisema walipomuuliza alikokuwa akielelea ndipo alipowajibu alikuwa akienda kujihifadhi kwa hakutaka kurudi tena kwenye nyumba baba yake kwa madai kuwa alikuwa akimnyanyasa na kumtesa pamoja kumuingilia kimwili bila kumpatia huduma yoyote.
Walisema kutokana na hali hiyo waliingiwa na huruma na kuamua kuripoti katika ofisi ya Kijiji ambapo kwa pamoja walimsaka mwanaume huyo na kufanikiwa kumpata na kisha kumfikisha katika vyombo vya dola huku taratibu za kumfanyia usafi binti zikiendelea kutokana na hali yake kudhoofu na kunuka mwili wake.
Akisimulia mkasa huo mbele ya waandishi wa habari binti huyo [19] alisema vitendo vya kikatili vilianza baada ya mama yake kufariki akiwa mdogo ambapo alilazimika kukatiza masomo akiwa darasa la sita shule ya msingi kiwanja kutokana na kukosa chakula na mahitaji ya shule kama sare na madaftari.
Alisema hali hiyo ilipelekea yeye kufanya vibarua kama kulima, kuuza bar na kuchimba dhahabu ili kujikimu kwa chakula yeye na wadogo zake wanne waliokuwa hawapati mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Aidha alisema baada ya kuchoshwa na vitendo hivyo binti huyo aliacha masomo na kuolewa Jijini Mbeya akiwa na miaka kumi na nne ambapo waliishi na mumewe kwa miaka mitatu ndipo Mumewe alipokamatwa kwa wizi kasha kufungwa ndipo yeye aliamua kurudi nyumbani kwa baba yake wakati huo akiishi Chalangwa akifahamika kwa jina la Maneno Pesambili Kanjanja.
“Baadae tulihamia kijiji cha Kiwanja huku baba akiendelea kunitesa na kukumbwa na ulemavu wa miguu na baba akawa ananifungia ndani na kuniingilia kimwili mbele ya wadogo zangu watatu kwa zaidi ya miezi miwili sasa licha ya ulemavu wa miguu” alilalamika binti huyo.
Aliongeza kuwa amekuwa akifanya ukatili pia amekuwa akimnyima chakula na maji pia alianza kumnyanyasa baada ya kuona ananuka sehemu za siri kutokana na kukosa maji ya kujisafisha wakati wa hedhi na kuanza kumtukana kuwa ni jinni linanuka.
Kutokana na ukatili huo wanachi hao walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji Gideon Kinyamagoha ambaye alimhoji Mtuhumiwa lakini hakuridhishwa na majibu ndipo alioamua kuwasilana na Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Chunya Theresia Mwendapole kwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii amekiri kupokea suala hilo na kutoa taarifa Polisi ambapo walifungua jalada la uchunguzi kwamba mwanaume huyo ameshindwa kuhudumia familia.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa alithibitisha kuweo kwa tukio hilo licha ya kukiri kuwa alipata taarifa kupitia kwa waandishi wa habari waliofika kufuatilia tukio hilo la unyanyasaji.
Hata hivyo Madusa alilazimika kufuatilia kwa kina jambo hilo na alipofika Kijijini hapo ambapo alikutana na Serikali ya Kijiji na Kata, Kaimu Mtendaji Kata Tegemea Kaminyoge alisema alimfahamu mtuhumiwa akiwa Chalangwa kabla ya kuhamia hapo.
Akiongea na Mkuu wa Wilaya binti huo alikiri kufanyiwa vitendo vya kikatili na baba yake kwa kunyimwa chakula na kuingiliwa kimwili.
Mkuu wa Wilaya, Madusa baada ya kujiridhisha na hali halisi ameliagiza Jeshi la polisi kubadilisha mashitaka ya kumwingilia kimwili badala la lile la awali la kushidwa kutoa matunzo kwa familia.
Aidha Madusa alimwagiza Afisa ustawi wa jamii kumpeleka hospitali binti huyo na kupimwa vipimo vyote pamoja na mtuhumiwa ikiwa ni sambamba watoto wengine watatu wa Maneno Pesambili wanaoishi hapo akiwemo wa kiume mwenye umri wa miaka sita aliyekatisha masomo na kuajiriwa kuchunga ng’ombe ili kubaini kama kuna magonjwa wameambukizwa.
Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa Serikali itahakikisha inasimamia kwa hali na mali matibabu ya binti huyo ili aweze kutibibiwa na kurejea katika hali yake ya awali.
“Nitoe wito kwa jamii tuendelee kushirikiana katika kundoa maovu katika jamii zetu kwa kuwafichua mapema wahusika kabla hawajaleta madhara, huyo tutamtibu na atapona hayo macho ni kwa ajili ya kufungiwa ndani kwenye giza pia mhusika kule ameshafika msiwe na wasiwasi” alisema Madusa.
Post a Comment
Post a Comment