Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al Shabaab limesema wapiganaji wake wameua wanajeshi kadhaa wa jeshi la Ulinzi la Kenya waliposhambulia kambi ya jeshi hilo iliyopo nchini Somalia leo hii huku taarifa kutoka jeshi la Kenya zikipuuza taarifa hizo na kusema kuwa wao ndio waliowaua wanamgambo waliotaka kufanya shambulio hilo.
Mseamji wa kundi la al Shabaab, kikundi ambacho mara nyingi kinashambulia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika (AU), amesema wanamgambo wao wameua wanajeshi zaidi ya 66 wa Kenya katika kambi iliyopo kusini mwa mji wa Kulbiyow, karibu na mpaka wa Kenya.
Msemaji huyo amekiri kuwa baadhi ya wanamgambo wa Al Shabaab wameuawa lakini hakutoa idadi yao.
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Kenya Luteni Kanali Paul Njuguna amekanusha madai ya kwamba al Shabaab imeua wanajeshi hao wa Kenya, lakini yeye pia hakusema idadi ya majeruhi.
Katika taarifa yake, amesema kuwa washambuliaji wa al Shabaab walitumia gari lililowekwa mabomu kujaribu kusababisha milipuko wakati wanataka kuvamia kambi hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) lakini wanajeshi wetu waliwazuia na kuwaua wengi wa wanamgambo hao,” alimalizia Luteni Kanali Njuguna kwa kusema kuwa shambulio hilo limefanyika alfajiri ya kuamkia leo.
Post a Comment
Post a Comment