Kituo Kikubwa cha Mafuta Mkoani Njombe Chafungwa Leo

Katika Picha ni Purukushani wakati kituo hicho kikifungwa Mjini Njombe,


Kampuni ya Mafuta ya Total Imekifungia Kituo Chake Cha Mafuta Cha Mjini Njombe Kutoa Huduma Baada ya Wakala Aliyepewa Kazi ya Kukiendesha Bwana Mexon Sanga Kudaiwa Kukiuka Masharti ya Mkataba.

Hatua ya Kukifungia Kituo Hicho Imefanyika na Kampuni ya Udalali ya Marcas Debt Collectors and Auction Mart Limited ya Jijini Dar Es Salaam Kutokana na Mkataba wa Wakala Huyo Kumalizika Pamoja na Kinga ya Miezi Sita Iliyotolewa na Mahakama Hapo Awali ya Kukatisha Mkataba Huo.

Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Bwana Richard Paul Amesema Kuwa Licha ya Kumalizika Kwa Mkataba na Kampuni ya Total Lakini Pia Wakala Huyo Amekuwa Akinunua Bidhaa ya Mafuta Nje ya Kampuni Ya Total Jambo Ambalo ni Ukiukwaji wa Mkataba.

Amesema Awali Walitaka Kukatisha Mkataba na Wakala Huo Lakini Mahakama Ikimwekea Kinga ya Miezi Sita Ambayo Hata Hivyo Imeisha Januari 20 Mwaka Huu.

Wakati wa Zoezi la Kukifungia Kituo Hicho Likifanyika Wakala Mexon Sanga Alifika na Mapanga na Kuanza Kukata Utepe Uliozungushiwa Kwenye Kituo Hicho Jambo Lililolifanya Jeshi la Polisi Kumkamata Pamoja na Dereva Wake na Kumpeleka Kituoni.

Jitihada za Kumpata Wakala Huyo Ziligonga Mwamba Baada ya Jeshi la Polisi Kumpeleka Korokoroni Huku Kamanda wa Polisi Akishindwa Kukutikana Kituoni Hapo na Baada ya Kumtafuta Kwa Njia Ya Simu Ilikata na 
Haikupatikana Tena.

Related Posts

Post a Comment