MAHAKAMA YASABABISHA KUSHUKA KWA THAMANI YA FEDHA KENYA

Shilingi ya Kenya yatajwa kushuka thamani dhidi ya dola ya Marekani baada ya Mahakama ya Juu ya Kenya kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Urais Leo Septemba 1, 2017.

Muda mchache baada ya Mahakama ya Juu ya Kenya kutoa uamuzi wake benki za kibiashara za Kenya zimeonesha kuwa shilingi ilikuwa 103.20/40 kwa dola, ikilinganishwa na 102.75/95 siku ya Alhamisi Agosti 31, 2017.

Biashara katika Soko la hisa la Nairobi ilisimama kwa muda kutokana na wafanyabiashara kuhofia kupoteza mitaji yao, hasa wawekezaji kutoka nje ya Kenya.

Mahakama ya Juu ya Kenya Leo Ijumaa asubuhi iliitangaza kufuta uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8, 2017 na kuamuru kufanyika kwa uchaguzi mwingine ndani ya siku sitisi (60). Mahakama imetengua ushindi wa Rais Uhuru Kenyata kwa hoja kuwa haukuwa halali kutokana na Tume ya Uchaguzi kuwa na makosa mengi na kuenda kinyume na sheria nyingi za uchaguzi.

Related Posts

Post a Comment