const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Aliyemuua mtoto wake bila kukusudia aachiwa huru - HABARI MPYA

..

Aliyemuua mtoto wake bila kukusudia aachiwa huru



Na John Walter -Manyara

Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara imemuachia huru kwa sharti la kutokufanya kosa lolote ndani ya miaka miwili Bi Rahma Shabani  Hussein mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa kitongoji  cha Kalangala kijiji cha Loiborsiret Wilayani Simanjiro kwa kosa la kumuua mtoto wake bila kukusudia.

Tukio hilo lilitokea  tarehe  2.9.2023  ambapo Mtoto aliyejulikana kwa Jina Faisal Alphonce mwenye umri wa mwezi mmoja aliuwawa na mama yake kufuatia kugandamizwa bila kujua baada yakuwa katika hali ya ulevi.

Akisoma Mashtaka mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Manyara Mhe. John Kahyoza, leo februari 1,2024  mwendesha Mashtaka wa Mkoa wa Manyara Chemma Maswi  amesema mshtakiwa ambaye ni mama wa marehemu, Siku ya tukio saa Saba Mchana alitoka nyumbani kwake kuelekea nyumbani kwa mama Asha ambaye huwa anauza pombe za kienyeji ambapo aliagiza pombe aina ya buza na akaendelea kunywa mpaka saa 11 jioni.

Alipofika nyumbani alimkuta Mtoto wake huyo wa mwezi mmoja amelala ambapo aliendelea kulala naye huku akiwa amemlalia bila kujua na alipostuka saa saba usiku kwa lengo la kumnyonyesha ndipo alipogundua kuwa mwanaye hayupo sawa kwani alikuwa akitokwa damu mdomoni na puani.

Baada ya kugundua alitoa taarifa kwa majirani ambapo walipomtazama waligundua alishafariki.

Jaji Kahyoza amesema mahakama imeamua kumuachia huru mshtakiwa kutokana na mazingira ya tukio lilivyokuwa.

Uchunguzi wa kitabibu uliofanywa na daktari wa zahanati ya Loiborsiret  Mohamed Utanga, ulibaini kuwa kifo cha mtoto huyo kilitokana na mgandamizo wa nguvu kutoka nje sehemu ya kichwa na kupelekea kukosa hewa.

Awali Wakili Thadei Lister aliyekuwa upande wa utetezi aliiomba mahakama ione huruma kwa mteja wake kwani ameshajutia kosa lake na alishaomboleza kifo Cha mwanaye akiwa kwenye mikono ya magereza na polisi,mahakama kwa muda mrefu.

Hukumu hiyo imeshuhudiwa na viongozi wa dini mkoa wa Manyara, mkuu wa wilaya ya Babati na wananchi ikiwa ni maadhimisho ya wiki na siku ya sheria nchini.

Newest Older

Related Posts

Post a Comment