Na John Walter-Manyara
Ikiwa leo 08/01/2024 wanafunzi katika maeneo mbalimbali nchini wakirejea shuleni kuendelea na masomo baada ya likizo ya mwisho wa Mwaka 2023 na Sikukuu ya Christmas na Mwaka Mpya.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amekuwa mtu wa kwanza kugonga kengele mapema saa 12 asubuhi katika shule ya Msingi Kateshi "A" kama ishara ya kuanza upya kwa masomo 2024 ambapo shule hiyo ilikuwa ikitumika kama kituo cha kupokelea misaada ya Waathirika wa Mafuriko Hanang.
Rc Sendiga pia ametembelea shule mbalimbali za msingi na Sekondari ambazo ziliathiriwa na Mafuriko wilayani humo kwa lengo la kujionea hali ilivyo pamoja na kutoa pole kwa wanafunzi pamoja na waalimu ambapo katika shule ya Msingi Jorodomu walifariki wanafunzi 15 huku shule ya Sekondari Ganana walifariki wanafunzi wawili
Katika hatua nyingine RC Sendiga ametoa siku tatu kuanzia leo kwa maafisa elimu msingi na Sekondari Kuhakikisha wanafunzi wote wanarejea shuleni hasa wale ambao hawajathiriwa na tukio la Mafuriko
Tukio la Mafuriko yaliyoambatana na tope lilitokea Disemba 03, 2023 na kupelekea vifo vya watu 89, majeruhi 139 pamoja na uharibifu wa Mali na vitu mbalimbali katika wilaya ya Hanang Mkoani Manyara ambapo Leo imetimia siku ya 37 toka kutokea kwa tukio hilo.
Post a Comment
Post a Comment