Sehemu ya ghorofa ya tano ya jengo la Kampuni ya Mkombozi Fishing and Marine Transoprt lililopo Kirumba
Mwaloni katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imeungua kwa moto ambao chanzo chake bado
hakijafahamika.
Jengo hilo linalomilikiwa na mfanyabiashara wa jijini Mwanza Kitana chacha ujenzi wake bado haujakamilika.
ITV ilifika katika eneo la tukio hilo na kukuta wananchi wakishirikiana na askari wa jeshi la zimamoto na
uokoaji Mwanza kuzima moto huo uliokuwa umeteketeza mbao zinazotumika kwa ujenzi wa ghorofa hilo, huku
Afisa mafunzo na habari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Mwanza Mkaguzi Msaidizi Gadaffi
Masoud akifafanua kuhusu tukio hilo.
Tukio hilo la moto limekuja ikiwa ni wiki tatu baada ya moto mkubwa kuteketeza sehemu ya nyuma ya nyumba
ya kulala wageni ya Shinyanga iliyopo mtaa wa Lumumba jijini Mwanza na kusababisha kifo cha mmiliki wa
jengo hilo Maduhu Masunga maarufu kama mzee Shinyanga pamoja na kuteketeza silaha mbili,kiasi kikubwa
cha fedha na mali mbalimbali ambazo thamani yake haikuweza kufahamika mara moja.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
Post a Comment
Post a Comment