Japokuwa katika msimu wake wa kwanza Epl baada ya kununuliwa kutoka Juventus hakuwa na kiwango bora sana kama mashabiki walivyotegemea lakini alicheza vizuri na akiisaidia United kubeba kombe la Europa.
Msimu ujao hakika anaweza kuwa bora sana na mashabiki wa Manchester United wakamfurahi sana Paul Pogba kama ambavyo mchezaji mkongwe wa timu hiyo ambae sasa ni mchambuzi wa soka Ryan Giggs anavyoamini.
Giggs anaamini kwamba msimu ujao wa ligi kuu ya Epl huenda wapinzani wa Paul Pogba wakawa katika wakati mgumu sana kwani kiwango cha Mfaransa huyo kinaweza kurudi katika level aliyokuwa nayo wakati akiwa Juventus.
Imani ya Giggs imekuja baada ya kiwango bora sana ambacho Pogba alikionesha wakati wa pambano la kimataifa la kirafiki kati ya Ufaransa na Uingereza pambano ambalo liliisha kwa Ufaransa kushinda mabao 3 kwa 2.
“Ukimuangalia alivyocheza dhidi ya Uingereza lazima utasisimkwa kama wewe ni shabiki wa United haswa ukiwaza kwamba huyu mchezaji atacheza hivi katika msimu ujao wa ligi anaweza kuwa hashikiki” alisema Giggs.
Wachambuzi wengine akiweomo Ian Wright ambaye naye alikuwa akiangalia mchezo huo alikiri kwamba kama kiwango alichokionesha Paul Pogba dhidi ya Uingereza atakileta katika ligi ya Epl baasi atawasha moto.
Post a Comment
Post a Comment