const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Kumbe Real Madrid wanamtaka Mbappe tangu kitambo sana. - HABARI MPYA

..

Kumbe Real Madrid wanamtaka Mbappe tangu kitambo sana.

Usiku wa jana kinda Kylian Mbappe aliwalaza mabeki wa timu ya taifa ya Uingereza na viatu baada ya kuwanyanyasa sana katika mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo, mchezo huo uliisha kwa Ufaransa kushinda mabao 3 kwa 2.

Baada ya mchezo huo Kylian Mbappe alielezea ni jinsi gani Real Madrid wamekuwa wakimtafuta na kutaka kumsajili toka akiwa na umri mdogo wa miaka 14 lakini hadi sasa klabu hiyo haijaacha kutaka kumsajili.

Mbappe ambaye timu za Chelsea,Manchester United na PSG alisema “wamekuwa wakijaribu kunisajili tangu nikiwa na umri wa miaka 14, nitakwenda mapumzikoni na familia yangu na tutajadili ni nini kitatokea baadae”

Inaeleweka Mbappe anavutiwa sana na Cristiano Ronaldo na huenda akavutiwa kucheza naye katika timu moja lakini amesisitiza kwamba yeye ni mchezaji wa Monaco na ana mkataba na timu hiyo lakini hana uhakika wa atakapocheza msimu ujao.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!


Related Posts

Post a Comment